Na Shomari Binda-Musoma
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Agnes Marwa amewasilisha utekelezaji wa ilani ya CCM ya miaka 5 huku akijivunia yale aliyo yafanya.
Uwasilishaji huo ameufanya leo mei 23,2025 kwenye kikao cha Baraza la UWT mkoa wa Mara lililofanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa.
Mbele ya wajumbe wa baraza hilo na madiwani wa viti maalum mkoa wa Mara lililoongozwa na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Mara Nancy Msafiri amesema ni mengi aliyoyatekeleza na kila ameshuhudia.
Amesema kama mbunge anayetokana na wanawake ni mengi amewafanyia ikiwa ni kuwawezesha kiuchumi kupitia vikundi vyao vya ujasiliamali.
Agnes amesema katika kipindi hicho cha miaka 5 licha ya kuwezesha wanà wake kiuchumi yapo mengi ya kijamii ambayo ameyafanya kwenye Wilaya zote za mkoa wa Mara kwenye sekta mbalimbali
Mbunge huyo amesema ameifikia jamii kwa misaada mbalimbali na uwakilishi wake bungeni umekuwa mzuri kwa kutoa michango mbalimbali ambayo bunge na serikali wamekuwa wakiifanyia kazi.
" Ndugu zangu kwenye kitabu hiki cha utekelezaji wa ilani kwa kipindi cha 2020/2025 ambacho kila mmoja anacho mengi nimeyaelezea ambayo mtakwenda kuyasoma taratibu.
" Ni imani yangu kwa yale niliyoyafanya muda ukifika nikichukua fomu mtanirudisha tena kwenye nafasi hii niweze kuwatumikia kwa kipindi kingine",amesema.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM mkoa wa Mara Nancy Msafiri amesema kazi zilizofanywa na mbunge huyo zinaonekana na ametekeleza vyema ilani ya uchaguzi.
Amesema kama Mwenyekiti wa jumuiya anajivunia uwakilishi wa wabunge wa viti maalum wa mkoa wa Mara Agnes Marwa na Ghati Chomete kwa mazuri waliyoyafanya.
Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa wa Mara Iddy Mkowa amesema wanawake wanapaswa kupendana na kudai amesoma utekelezaji wa wabunge wa viti maalum mkoa wa Mara na wanastahili kupongezwa.
0 Comments