Header Ads Widget

WAZIRI NDEJEMBI: HATUA KALI ZINAENDELEA KUCHUKULIWA KWA WATUMISHI WANAOKIUKA SHERIA ZA ARDHI.


Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima App Dodoma

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deo Ndejembi, amesema kuwa wizara yake itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya watumishi wa umma wanaokiuka taratibu na sheria za usimamizi wa ardhi nchini.

Akizungumza leo Mei 23,2025 wakatia akieleza mfanikio ya serikali ya awamu y sita Waziri Ndejembi amesema tayari watumishi wengi wamesimamishwa kazi na wengine kufukuzwa baada ya kuthibitika kujihusisha na vitendo vinavyokiuka maadili ya kazi na kusababisha migogoro ya ardhi.

"Hatua zimekuwa zikichukuliwa kwa watumishi wanaokiuka utaratibu Wakigundulika, tunawaondoa mara moja tayari wapo wengi tumeishawasimamisha na kuwafukuza kazi, " Amesema

Na kuongeza " tunaendelea kuwa wakali kwa yeyote atakayesababisha mgogoro au kukiuka sheria na taratibu zilizopo," amesema Mhe. Ndejembi.

Waziri huyo amesisitiza kuwa serikali haitamvumilia mtumishi yeyote anayehujumu haki za wananchi au kushiriki katika njama zinazohatarisha usalama na utulivu wa umiliki wa ardhi.

Amehimiza watumishi wote wa sekta ya ardhi kuzingatia weledi, uwajibikaji, na uadilifu katika utendaji wao wa kila siku.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI