Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Cyprian Luhemeja, ameshuhudia zoezi la usafishaji wa Ziwa Victoria katika maeneo yaliyoathirika na gugu maji, kuanzia Busisi wilayani Sengerema hadi Kigongo Feri wilayani Misungwi, mkoani Mwanza, tarehe 15 Mei 2025.
Zoezi hilo linaendelea kufanyika kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo nguvu kazi ya vijana wanaotumia mapanga pamoja na matumizi ya mtambo maalum wa kisasa ujulikanao kama Watermaster, wenye uwezo wa kusafisha na kuchimba kina chamaji kwa wastani wa eka moja kwa siku
Katika kuhakikisha jitihada hizi zinaendelezwa kwa ufanisi zaidi, serikali imechukua hatua za ziada ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mitambo mingine mitatu ya kisasa ambayo kwa sasa ipo katika hatua za awali za uwasilishaji.
0 Comments