Header Ads Widget

KIJANA BODA BODA AFUMANIWA AUWAWA KWA KUKATWA NYETI ,MAMIA WAANDAMANA


NA SHAMILA RAJAB MATUKIO DAIMA MEDIA IRINGA 

Mamia ya vijana wanaojishughulisha na kazi ya kuendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wamefunga mitaa mbalimbali ya mji wa Iringa leo, wakati wakisindikiza mwili wa mwenzao, Abisai Mhando, ambaye aliuawa kikatili kwa kukatwa sehemu za siri, tukio linalodaiwa kufuatia fumanizi.

Katika mahojiano na Matukio Daima Media  wakati wa shughuli za mazishi, baadhi ya madereva wa pikipiki waliomfahamu marehemu walieleza huzuni yao na jinsi walivyoshirikiana naye katika shughuli za kila siku.


Awesi Mwangamila, rafiki wa karibu wa marehemu, alisema:
“Mbali ya kuwa marafiki, Mhando pia alikuwa jirani yangu wa karibu. Tulishirikiana naye katika mambo mengi.

 Alikuwa mtu wa watu, asiye na makuu. Kifo chake kimeniumiza sana. Nasikitika kwa jinsi alivyopoteza maisha, na naomba Mungu ampunguzie adhabu ya kaburini.”

Julias Kiyeyeu, dereva wa pikipiki katika kituo cha Ipogoro, naye alieleza.


“Marehemu nilimchukulia kama mdogo wangu. Kifo chake kimeniumiza sana. Ingawa hatujajua undani wa tukio lote, ni muhimu tukakataa kuchukua sheria mkononi. Tujifunze kupendana na kuvumiliana.”

Majirani wa marehemu walieleza kuwa enzi za uhai wake, Abisai alikuwa kijana mtulivu, na wametoa wito kwa vijana wa kizazi hiki kujifunza kutokana na tukio hilo ili kuepuka matukio ya aina hiyo katika jamii.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mtaa alikokuwa akiishi marehemu alilaani vikali tukio hilo akilitaja kuwa ni tendo la kikatili.


“Ni jambo la kusikitisha sana. Ninawaomba wananchi waache tabia ya kujichukulia sheria mkononi. Tunapaswa kuendelea kushikamana kama jamii, hasa tunapokumbwa na matatizo ya aina hii.”

Abisai Mhando alizaliwa mwaka 1995 na alikuwa dereva bodaboda katika eneo la Ipogoro, Iringa. 

Alipoteza maisha siku ya Jumatatu baada ya kudaiwa kufumaniwa na mume wa mwanamke anayedaiwa kuwa mke wa mtu, na kushambuliwa kwa kukatwa sehemu za siri hali iliyosababisha kifo chake.TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI