Na Fatma Ally Matukio na Habari App
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni amesema kuwa maonyesho ya mwaka huu yamekua na mwamko mkubwa ikilinganisha na miaka iliyopita.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Mhansi Sangweni amesema kutokana na kuwepo kwa mazingira wezeshi, amani na utulivu shughuli za uzalishaji katika mkondo wa Juu wa Petrol kwenye nyanja ya ajira imeongezeka kutoka asilimia 55 hadi 85.
Aidha, amewata metoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika masuala ya Nishati Safi kutokana na kuwepo mikakati imara, mazingira wezeshi, amani na utulivu inayotoa fursa kwa maendeleo ya kiuchumi.
"Tangu mwaka 2017 tumekuwa tukishiriki maonesho haya na mwaka huu yamekuwa wa mazuri kutokana na kuendeshwa kidigitali zaidi na tutaendelea kushiriki kwa mafanikio makubwa na kwa mwaka huu tumepata maswali mazito kutoka kwa wananchi wanaofika kutembelea banda letu kuhusu nishati safi na tumewajibu kwamapana na ninaamini wameridhika," amesema Mhandisi Sangweni.
"Tunamshukuru Rais, kwani amefanya kazi kubwa katika uwekezaji katika mamlaka hii kwani kuanzia mishahara na uwepo wa mazingira wezeshi na rafiki kwa wawekezaji, hivyo ni wakati wao wawekezaji kuitumia nafasi hiyo kuja kuwekeza hapa nchini hususan katika Nishati Safi,"amesema.
Amesema kuwa,kwa sasa wapo katika mchakato wa kuchimba visima vitatu vya gesi asilia mkoani Mtwara ambapo uchimbaji huo unaotarajia kuanza mwezi Nov mwaka huu, huku wakitarajia kuongeza uzalishaji wa gesi asilia kutoka kitalu cha Mnazi Bay kwa zaidi ya ujazo wa milioni 30 kwa siku jambo ambalo litakuwa ni mafanikio ya kujivunia.
Ameongeza kuwa, kati ya kampuni 10 zinazoshughulika na utafutaji mafuta na gesi sita ni za kitanzania na hiyo inatokana na kuwepo mpango wa mkakati wa kuhakikisha vyuo vya Tanzania vinafundisha kozi za mafuta na gesi na wahitimu wanapomaliza masomo yanaingia moja kwa moja kufanya shughuli hizo.
[7/10, 9:22 AM] Francis Godwin: ingekuwa na maiki yetu inaonekana ingepanda fasta
0 Comments