Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka usiku wa jana mei 17,2025 ameufatilia mchezo wa timu ya RS Birkane na Simba kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo Manispaa ya Musoma.
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya timu hizo uliochezwa katika Manispaa ya Birkane nchini Morocco ulishuhudia timu ya Simba ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.
Mkuu huyo wa Wilaya alifunga "projector" ÿa screen kubwa kuwapa fursa wananchi na mashabiki wa soka kufatilia mchezo huo na kupata burudani mbalimbali.
Akizungumza kablà ya kuanza kwa mchezo huo mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amesema lengo la kutazama mchezo huo pamoja na kuweka burudani ya muziki ni kuendelea kuufanya mji wa Musoma kuchangamka kwa matukio.
Amesema huo ni muendelezo ambao licha ya kuhamasisha wananchi kufanya shughuli za kiuchumi suala la kula bata na kupata burudani ni sehemu ya maisha kwa wananchi wa Musoma.
Mkuu huyo Wilaya ya Musoma amesema kuuchangamsha mji ni pamoja na kufanyika kwa matukio kama hayo ya kukutana pamoja ili kuweza kufurahi.
Kwa upande wao wananchi walioshuhudia mchezo huo uwanjani hapo wamemshukuru mkuu huyo wa Wilaya kwa kuwakutanisha pamoja kuufatilia mchezo huo.
Mkondo wa pili wa mchezo wa fainali wa kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba na RS Berkane utafanyika mei 25,2025 hapa nchi kwenye uwanja New Amani Complex visiwani Zanzibar au uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salam.
" Leo tumekuta pamoja kufatilia mchezo huu wa fainali hapa kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo na lengo ni moja kuuchangamsha mji wetu kwa kukutana pamoja kwa matukio kama haya.
" Nawashukuru sana wananchi kwa kujitokeza na hapa kuna vinywaji tutumie na wakati mwingine itaandaliwa nyama choma ya kutosha tule bata baada ya kazi",amesema.
0 Comments