Na Shemsa Mussa -Matukio daima,Kagera
Hatima ya ukamilishaji wa ujenzi wa Barabara njia Nne Bukoba Mkoani Kagera unatalajiwa Mwezi November 15/2025.
Akizungumza kuhusu maendeleo ya mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Kagera, Mhandisi Ntuli Mwaikokesya, amesema kuwa ujenzi huo ulikwama kwa muda hali iliyozua maswali mengi kutoka kwa wananchi
Aidha amesema Ujenzi huo wa barabara njia nne kutoka Makutano ya barabara ya Rwamishenye hadi Makutano ya barabara ya stendi ya mabasi yenye urefu wa kilomita 1.6, unatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba 15 mwaka huu.
“Wananchi wamekuwa na maswali pengine ya sintofahamu ni lini Barabara hii itakuwa tayari kwa matumizi ila sisi kama Tanroad) hatujalala kazi inaendelea na hapa tunaendelea ukarabati wa daraja Letu la kanoni ili turahisishe kazi,amesema Mwaikokesya "
Kuhusu uwezekano wa kujenga daraja mbadala kwa ajili ya watembea kwa miguu, Mhandisi Mwaikokesya ameeleza kuwa hilo halipo katika mkataba wa ujenzi hivyo Kwa sasa, wananchi wataendelea kutumia njia ya kuzunguka kupitia Nyakanyasi, Kashura pamoja na Kashozi Road.
0 Comments