Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma
Wizara ya Viwanda na Biashara imewasilisha ombi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla ya shilingi bilioni 135.7 kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake katika mwaka wa fedha 2025/2026.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo leo bungeni, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Jafo, amesema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 93.9 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 41.8 ni kwa matumizi ya maendeleo.
Katika fedha za matumizi ya kawaida, Dkt. Jafo alifafanua kuwa shilingi bilioni 75 zitatumika kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi wa wizara hiyo, huku shilingi bilioni 18 zikiwa ni kwa matumizi mengineyo.
Aidha, kati ya shilingi bilioni 41.8 zinazotarajiwa kutumika kwa matumizi ya maendeleo, Waziri Jafo amesema shilingi bilioni 14 zinatoka kwa wahisani wa maendeleo (fedha za nje), huku kiasi kilichobaki kikiwa ni fedha za ndani.
Waziri huyo amesema fedha hizo zitasaidia kuendeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ya viwanda, kukuza biashara za ndani na nje, pamoja na kuimarisha mazingira wezeshi ya uwekezaji nchini.
0 Comments