Header Ads Widget

CHARLESY HILARY AFARIKI DUNIA

 


Dunia  imekutwa na majonzi makubwa Alfajili ya leo kutokana kifo cha aliyewahi kuwa mtagazaji wa BBC na  Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary Nkwaga, kilichotokea alfajiri ya leo, Mei 11, 2025.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya uhakika Charles Hilary amefariki dunia ghafla alfajiri ya leo Mei 11 baada ya kuugua kwa muda mfupi na wakati akikimbizwa Hospital ya Muhimbili tawi la Mlonganzila alifikwa na mauti.

Charles amefanya kazi katika vyombo mbali mbali baada ya kustaafu BBC kwa upande wa Tanzania amefanya kazi Azam Media akiwa Mkuu wa Idara ya redio ya UFM.

Baada ya hapo, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar, nafasi ambayo aliitumikia hadi mauti yalipomkuta.

  Charles Hilaryametumikia Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati huo likijulikana kama Redio Tanzania.

Alianza kazi ya utangazaji zaidi ya miongo miwili iliyopita, na ameacha alama isiyofutika katika vyombo mbalimbali vya habari nchini na nje ya nchi.

 Charles pia alifanya kazi na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), akiitangaza Tanzania vyema katika jukwaa la kimataifa.

Mbali na taaluma yake ya uanahabari, Charles alijulikana kwa ucheshi, utu na moyo wake wa kusaidia wengine, hasa waandishi chipukizi na watangazaji waliokuwa wakianza safari zao.

Alikuwa mwalimu, mshauri na kiongozi mwenye maono katika tasnia ya habari.


Kifo chake ni pigo kubwa si tu kwa familia, ndugu na marafiki, bali pia kwa sekta nzima ya habari na mawasiliano nchini. Tanzania na Dunia  Nenda salama Charlesy Hilary umevipiga vita vilivyo vizuri Mwendo umemaliza salama 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI