Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI PROFESA PATRICK NDAKIDEMI ASHIRIKI MAZISHI YA WATU WATATU WALIOFARIKI KWA KUDONDOKEWA NA NGEMA KATIKA KATA YA MBOKOMU



NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameshiriki katika mazishi ya watu watatu Easther Mlinga (50), mtoto wake Emanuel Fredy Mlinga (14) na Zaina  Ladston (65) waliofariki kwa mafuriko. 


Umauti uliwapata marehemu hao Mei 6 mwaka huu usiku kufuatia mvua kubwa zinazonyesha mkoani Kilimanjaro ambapo mafuriko yalisababisha ngema ya udongo kuwafukia kwenye makazi yao wakiwa wamelala.



Mazishi hayo yalihudhuriwa na mamia ya wananchi wakiwemo viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Nzava na viongozi waandamizi wa wilaya na Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Moshi.


Chama Cha Mapinduzi kiliwakilishwa na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Moshi vijijini ikiongozwa na Katibu wa CCM Wilaya, Ramadhani Mahanyu. 



Ibada ya mazishi ilifanyika katika Usharika wa Fukeni ikiongozwa na mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Kati la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mchungaji Javason Mrema.



Akitoa salamu za rambirambi Mbunge alitoa pole kwa Familia zote mbili zilizofiwa, ndugu jamaa na marafiki.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI