Header Ads Widget

ZIMAMOTO NA UOKOAJI WAWAOKOA WATOTO WATANO WALIOZIDIWA NA MAJI MTO MOROGORO

 JESHI la zimamoto na Ukoaji Mkoa wa Morogoro limefanikiwa kuwaokoa watano waliokuwa wamekwama kwenye mto Morogoro baada ya kuzidiwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha 

Miongoni mwa watoto hao,   wawili walikwama kwenye mto Morogoro walikokwenda kwaajili ya kufua baada ya kuzingirwa na maji huku vijana watatu wakikwama Mtoni baada ya kupiga mbizi kuwafuata Ili wawaokoe na wao kuzidiwa na maji.

Awali watoto waliokuwa wamezingirwa ghalfa na maji, walipiga kelele  kuomba msaada wa wananchi na vijana watatu walipiga  mbizi  mtoni kujaribu kuwaoa bila mafanikio baada ya wao pia kujikuta wamezingirwa na maji yaliyozidi kuongezeka na kushindwa pia kutoka kujiokoa.

 Wananchi walitoa taarifa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Morogoro na kuomba msaada wa haraka wa uokozi ambapo askari walifika eneo la tukio kwa wakati na kuwaokoa.

Habari na  Matukio daima App.

JESHI la zimamoto na Ukoaji Mkoa wa Morogoro limefanikiwa kuwaokoa watoto watano waliokuwa wamekwama kwenye mto Morogoro baada ya kuzidiwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha 

Miongoni mwa watoto hao,   wawili walikwama kwenye mto Morogoro walikokwenda kwaajili ya kufua baada ya kuzingirwa na maji huku vijana watatu wakikwama Mtoni baada ya kupiga mbizi kuwafuata Ili wawaokoe na wao kuzidiwa na maji.

Awali watoto waliokuwa wamezingirwa ghalfa na maji, walipiga kelele  kuomba msaada wa wananchi na vijana watatu walipiga  mbizi  mtoni kujaribu kuwaoa bila mafanikio baada ya wao pia kujikuta wamezingirwa na maji yaliyozidi kuongezeka na kushindwa pia kutoka kujiokoa.

Wananchi walitoa taarifa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Morogoro na kuomba msaada wa haraka wa uokozi ambapo askari walifika eneo la tukio kwa wakati na kuwaokoa.

Jeshi la Zimamoto na uokoaji Morogoro wakiongozwa  Sajenti Ramadhan Katonga walifanikiwa kuwaokoa watoto hao  baada ya kuingia majini akiwa na vifaa mbali mbali vya uokozi.

Akizungumza baada ya uokozi, Sajenti Katonga amewataka wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao hasa wakati huu wa mvua kwani hazitabiriki na wakati mwingine  huwa kubwa na kuleta madhara.

Sajenti Katonga akaishukuru Serikali kupitia kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini,  CGF John Masunga kuliwezesha Jeshi hilo vifaa mbalimbali vya uokozi na kuendelea kutoa mafunzo ya maokozi kutoka ndani na nje ya nchi kwa askari wake.

Nao Baadhi ya wananchi Eline Goodluck na Carlos Iddi walishukuru  Serikali kupitia Jeshi la Zimamoto mkoa wa Morogoro kuwahi kwa wakati eneo la tukio na kunusu maisha ya watoto hao ambao huenda wangeweza kupoteza maisha kama wasingesaidiwa kwa wakati 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments

MAGAZETI

NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI