Rais wa Ukriane, Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemwalika Donald Trump kuzuru nchi yake kabla ya makubaliano yoyote na Urusi yakumaliza vita.
"Tafadhali, kabla ya aina yoyote ya maamuzi, aina yoyote ya mazungumzo, njoo uone watu, raia, wapiganaji, hospitali, makanisa, watoto walioharibiwa au waliokufa," Zelensky alisema katika mahojiano ya programu ya Dakika 60 ya CBS.
Mahojiano hayo yalirekodiwa kabla ya kombora la Urusi kushambulia mji wa Sumy, na kuua watu 34 na wengine 117 kujeruhiwa.
Urusi haijatoa maoni.
Trump alisema alikuwa ameambiwa kuwa ilikuwa ni shambulizi la kimakosa, bila kutaja kama kauli hii imetolewa na Moscow.
Kaimu Kansella wa Ujerumani, Friedrich Merz, aliishutumu Urusi kwa kufanya uhalifu wa kivita.
Hapo awali, mjumbe maalum wa Trump nchini Ukraine, Luteni Jenerali mstaafu Keith Kellogg, alisema shambulio hilo limevuka "mstari wowote wa adabu".
Walakini, inabakia kuonekana ikiwa Trump atakubali mwaliko wa Zelensky.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema "amefadhaika sana na kushtushwa" kujua kuhusu shambulio hilo la kombora.
"Mashambulizi dhidi ya raia na vitu vya kiraia yamepigwa marufuku chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, na kwamba mashambulizi yoyote kama hayo, popote yanapotokea, lazima yakomeshwe mara moja", aliongeza.
Guterres alisisitiza uungwaji mkono wa Umoja wa Mataifa kwa "juhudi za maana kuelekea amani ya haki, ya kudumu na ya kina ambayo inasimamia kikamilifu uhuru wa Ukraine, kama taifa".
Shambulio la mara mbili la makombora la Jumapili lilikuwa shambulio baya zaidi dhidi ya raia nchini Ukraine mwaka huu.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa karibu watu milioni saba wa Ukraine wanaishi kama wakimbizi.
0 Comments