Header Ads Widget

AFRIKA KUNUNUA MASHINE YA PLAYSTATION 5 KWA BEI YA JUU - SONY


Huku ushuru wa kimataifa wa Trump kwa bidhaa za mataifa zaidi ya 60, Shirika la Sony limetangaza kuongeza bei ya Playstation 5 katika masoko ya Ulaya, Uingereza, Australia na New Zealand.

Muungano wa teknolojia na burudani nchini Japani unasema "mazingira yenye changamoto ya kiuchumi" yanachangia hatua hiyo, ikitoa mfano wa mfumuko wa bei na viwango vya kubadilisha fedha vinavyobadilikabadilika.

Bei ya PlayStation 5 bila diski imepanda hadi euro 499.99 (US$569.59), kampuni hiyo inasema.

Kifaa hicho kitagharimu £429.99 (US$566.90) nchini Uingereza.

Kulingana na Reuters, hii ni 11% na 10% ya kupanda kwa bei hiyo.

Wateja nchini New Zealand na Australia wataona kupanda kwa bei ya mashine hiyo, pamoja na PS5 ya kawaida yenye kiendeshi cha Blu-ray.

Kampuni hiyo inasema kutakuwa na ongezeko la bei katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika, bila kutoa maelezo.

Michezo ya PS5 huendeshwa kwa njia ya diski au kwa kupakuliwa kutoka kwenye duka la mtandaoni la PlayStation Network.

Inaweza kutumika kwa kucheza michezo ya video, kutazama video, na kutumika kama kituo cha burudani cha nyumbani.

Ni mojawapo ya vituo vya michezo ya video vya kizazi kipya kinachopatikana sokoni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI