Na Pamela Mollel,Arusha
Wataalamu wanaohusika katika usalama wa mitandao kutoka Tanzania na nje ya Nchi wamekutana katika jukwaa la nne la pamoja la kujadiliana namna ambavyo mifumo itakuwa mathubuti katika kukabiliana na changamoto za kimtandao Duniani
Akizungumza katika jukwaa la nne,Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Tanzania Dkt Nkundwe Mwasaga anasema kuwa wamekuwa wakikutana na wataalamu wa mitandao kutoka Tanzania na Nje ya nchi ili waweze kujadiliana na kuweka maazimio ya kuboresha usalama wa mitandao .
Ameongeza kuwa kila ifikapo Aprili ya kila mwaka wamekuwa wakikutana na wataalamu wa mitandao ili kuweza kubadilishana utaalam pamoja na kupeana mrejesho wa mambo mbalimbali
"Eneo la usalama wa mitandao ni eneo ambalo linabadilika kila wakati hivyo ni muhimu kuwa na mifumo mathubuti"Ameongeza Dkt.Mwasaga
Kwa upande wake Afisa Usalama mtandao kutoka Benki ya CRDB,Robert Karamagi anasema kuwepo kwa makongamano kama hayo itasaidia Tanzania kuwa makini na wale wadukuzi wa mitandao
"Kwa namna ambavyo teknolojia ya mitandao inakuwa kwa kasi kubwa inahitajika elimu kwa jamii kujua namna ya kukabiliana na tishio lolote la kimtandao
Naye mtaalamu wa usalama mtandao na uchunguzi wa makosa mtandaoni Yusuph Kileo akiwasilisha mada ya uhalifu wa mitandaoni anasema kuwa jukwaa hilo ni muhimu kwani linajadili changamoto za kimitandao na kuzitafutia uvumbuzi.
Anaongeza kuwa tafiti zinaonyesha kuwa uhalifu mitandaoni unagharimu Dunia Dola Trilioni 10.5 kila mwaka hali ambayo inaogopesha
"Taasisi nyingi zinakumbana na changamoto za kimtandao ikiwemo kuibiwa taarifaa au fedha"Anasema Kileo
Mtaalamu wa mifumo ya Tehama kutoka IPP media Eng.Moses Fumbuka anasema kuwa kazi nyingi zinafanyika kupitia mifumo kwa asilimia 90
"Kwa hali ilivyo sasa huwezi kufanya chochote hivyo ni muhimu kuelewa mifumo inavyofanya kazi lakini hasa usalama wa mifumo "Anasema Eng.Fumbuka
0 Comments