Header Ads Widget

TETESI ZA SOKA IJUMAA: MAN CITY WAMTAKA UDOGIE WA SPURS

 


Manchester City wamemuongeza mlinzi wa kushoto wa Tottenham na Italia Destiny Udogie, 22, kwenye orodha fupi ya wachezaji wanaotarajiwa kusajiliwa huku wakipania kuimarisha nafasi ya mlinzi wa pembeni msimu huu. (Fabrizio Romano)

Meneja wa Lens Mwingereza aliyezaliwa Ubelgiji, Will Still, 32, ni miongoni mwa wanaowania kuwa meneja mpya wa Southampton kufuatia kuondoka kwa Ivan Juric mapema wiki hii. (Talk sport)

Arsenal, Chelsea, Liverpool, Newcastle na Spurs wamekutana au kufanya mazungumzo na wawakilishi wa mlinzi wa Uhispania mzaliwa wa Uholanzi Dean Huijsen, kabla ya uamuzi kufanywa kuhusu hatma ya mchezaji huyo wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 19. (Athletic)


West Ham wanafikiria kumnunua mlinda lango wa Southampton na Uingereza Aaron Ramsdale, 26 msimu wa joto. (Times )

Real Betis wanashikilia pauni milioni 35 huku Chelsea ikiongezajuhudi za kumnunua winga wa Uhispania Jesus Rodriguez, 19. (Mail, external)

Newcastle inajiandaa kuwasilisha dau la kumnunua ofa kipa wa Burnley James Trafford, 22, na inataka kumsajili Muingereza mwenzake Dominic Calvert-Lewin, 28, huku mkataba wa mshambuliaji huyo wa klabu ya Everton ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider )

Klabu ya Uholanzi ya PSV Eindhoven ina nia ya kutaka kumnunua winga wa Ipswich Muingereza Jack Clarke, 24, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Atalanta itatarajia kuanza ofa ya zaidi ya £51m (euro milioni 60) kwa mshambuliaji wa zamani wa Everton Ademola Lookman, 27, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Italia mwishoni mwa msimu huu. (Calciomercato)

Barcelona wamepunguza shauku yao ya kumnunua mlinzi wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Jonathan Tah, 29, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Bundesliga unamalizika tarehe 30 Juni. (Sport )


Kocha wa Genoa Patrick Vieira yuko mbioni kuwa kocha mpya wa Roma, huku kiungo huyo wa zamani wa Arsenal na Ufaransa akiwa kwenye orodha ya wachezaji wanne wanaowania kibarua hicho. (Sky Sport Italia )

Mkurugenzi wa soka wa Barcelona Deco amemteua mchezaji wa kimataifa wa Uhispania wa Real Sociedad Alex Remiro, 30, kuchukua nafasi ya Mjerumani Marc-Andre ter Stegen, 32, kwa nafasi ya mlinda lango wa klabu hiyo. (Catalunya Radio)

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI