Baadhi ya wageni wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi ambao ni Wenyeviti, Makatibu na Wakatibu Wenezi (CCM) ngazi ya Matawi kutoka Tarafa ya Isimani, Jimbo la Ismani walipohudhuria shughuli za Bunge wakati wa Kikao cha 15 cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 la Bajeti linaloendelea.
Wageni hao kutoka Mkoa wa Iringa walitembelea Bunge leo tarehe 30 Aprili, 2025 Jijini Dodoma.
Aidha, wageni hao walipata fursa ya kushiriki mafunzo kuhusu shughuli za Bunge zinavyofanyika katika ukumbi wa Msekwa na kufanya ziara ya kutembelea Mji wa Serikali- Mtumba.
0 Comments