Header Ads Widget

SEKTA YA SUKARI YAENDELEA KUTOA MCHANGO UKUAJI UCHUMI NCHINI.



📌WATAALAMU WA MIWA NA SUKARI NCHINI WAKUTANA KUJADILI NAMNA BORA YA KUONGEZA TIJA KATIKA UZALISHAJI


Na Lilian Kasenene,Kilosa Morogoro

Matukio DaimaApp 


PAMOJA na uwepo wa changamoto mbalimbali kwenye sekta ya sukari, Sekta hiyo bado imeendelea kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi nchini na maisha ya watu kwa ujumla ikiwemo kutoa ajira kwa vijana. 


Mkurugenzi wa uhamasishaji, uendelezaji wa teknolojia na ushiriikiano wa kitaaluma(Director of Technology Transfer and Partinership(DTTP) kutoka Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania(TARI) Dk Sophia Kashenge alisema hayo wilayani Kilosa, alipomwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo kwenye kongamano la wadau na wataalamu wa Sukari lililofanyika Chuo cha Sukari cha Taifa.


Dk Kashenge alisema sekta hiyo pia inachangia usalama wa chakula,na kwamba kama zilivyo sekta nyingine,suala la kupambana na changamoto zilizopo katika sekta hiyo ni muhimu hasa katika mabadiliko ya tabia nchi lakini kubwa zaidi ni ushindani uliopo katika soko, lakini uwepo wa wataalamu wa sukari nchini inaipa faraja serikali kuwa kuna nguvu kubwa katika uzalishaji.


‘Kipindi cha nyuma vijna wengi hawakuwa na hari ya kilimo hivyo palipo na mkusanyiko wa sayansi na teknolojia ndipo panachukua nafasi katika kuhakikisha panakuwa na mabadiliko chanya katika kukabiliana na changamoto zinazotukabili,”alisema.


Aidha Dk Kashenge alieleza kuwa wataalamu wanakazi kubwa ya kufanya ya kuhakikisha changamoto zilizopo zinaisha, aliongeza kuwa tafiti zinafanyika lakini kinachokosekana na uamishaji wa majibu ya utafiti na majaribio yanayofanyika ili yaende sasa kusaidia katika matumizi makubwa ya viwanda,kupunguza gharama za uzalishaji,kuboresha teknolojia mbalimbali zinazofanya uchakataji na hatimae kuhakikisha sukari ya Tanzania inafanya vizuri kwenye soko.


Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha sukari inashika kasi katika teknolojia ambapo alitoa mfaano wa kuwa kwa sasa kuna sgir centers 15 ambazo zinasaidia kwenye kilimo hivyo fedha za wafadhili kuzipata moja kwa moja ni vugumu hivyo ni vyema kama wataalamu lazima kuungana katika kilimo kwa umoja ili kuwa na nguvu ya pamoja.


Alipongeza Bodi ya sukari Tanzania kwa kusimamia kikamilifu juu ya upanuzi wa viwanda vilivyopo, uanzishwaji wa miradi mipya mblimbali ya sukari ikiwemo Bagamoyo na Mkulazi, vitalu vya mbegu bora kwa ajili ya wakulima wadogo, kuongeza matumizi ya Tehama katika kilimo cha miwa,kuweka sheria rafiki zinazovutia wawekezaji, usimamizi mahili wa soko la ndani,kuhimalisha na kuanzishwa kwa masomo ngazi ya stashahada ya uanzishaji sukari, na kilimo cha miwa kukuwa.


“Uwepo wa jitihada hizo umepelekea kuongeza uzalishaji wa sukali kutoka tani 294,000 kwenda tani 460,000 haya ni mafanikio makubwa,’alisema.


Pia mkurugenzi huyo alisema matumizi ya teknolojia hafifu hasa kwa wakulima wadogo pia inachangia uzalishaji wa sukari kuwa mdogo,akawataka wataalamu kutoa elimu ili tija ionekane na serikali inatambua  umuhimu wa jitihada zao na aliipongeza jumuiya ya wataalamu wa miwa na sukari wakiwa kama wadau muhimu kutokana na umuhimu huo akaeleza kuongoza nguvu katika maeneo ya mafunzo ili uzalishaji uendane nateknolojia zilizopo.


Rais wa jumuiya ya wataalamu wa miwa na sukari nchini(TSSCT) walioandaa kongamano hilo, Fihiri Achi alisema wameendelea kuwa chachu ya kuchagiza tafiti katika tasnia ya sukari na miwa wakiamini bila tafiti hakuna bunifu za kuongeza uzalishaji wa mbegu bora na teknolojia.


“Sisi kama wataalamu tunaohusika shaambani na viwandani tunaangalia ni changamoto gani tunakutana nazo mfano upande wa wakulima wadogo matumizi ya Tehama ni madogo kwa sababu bunifu za ndani hazija endelezwa na hii inafanya wakulima kuendelea kupata tija ndogo, kama wadau tumejikita kuhakikisha kwamba bunifu za ndani tutazitumia na kuzipeleka kwa wadau wote,”alisema Achi


Achi alieleza kuwa wao kama chama wameanzisha harakati za kushawishi wadau na mamlaka za serikali ambazo ndizo zenye karakana kutamani wakulima wapatie vifaa vinavyotumika kwa teknolojia.


“Chama kufanya kazi yake ni kuhakikisha serikali inaongeza azma yake ya kuongeza sukari,alisema


Mkurugenzi mkuu wa bodi ya sukari Prof Kenneth Bengesi alizungumzia mazingira tulivu ya uwekezaji yatakavyosaidia nchi kuondokana na uhaba wa sukari,alisema tasnia ya sukari imekuwa na maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka ya karibuni hasa awamu ya sita kwamba miaka ya nyuma kulikuwa na changamoto lakini zimekuwa zikitatuliwa.


Alisema utatuzi wake umekuwa ukifanyika kwa ushirikiana na serikali, wawejezaji(sekta binafsi), wanateknolojia wa sukari na hiyo ni kutokana na bunifu za teknolojia mbalimbali ambazo zinatoa majibu ya changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo katika tasnia hiyo.


“Hii yote imetokana na sababu zifuatazo ni kutokana na Serikali imeweka mazingira rafiki ya kuwahakikishia wawekezaji waliopo kufanya upanuzi wa viwanda, mashamba na kuwa na malighafi ya kutosha ili kuweza kuendana na upanuzi wa viwanda kuwa na uwezo wa kusaga miwa,”alisema.


Katibu mtendaji wa Tssct Mwanaidi Jaffery alisema wataalamu wa miwa na sukari wamekuwa wakipata ushirikiano kutoka kwa serikali kupitia taasisi zake ili kuhakikisha wanakutana na kutimiza na kutekeleza malengo wanayopaswa kufanya.


Kwa sasa uzalishaji wa sukari umeongezeka mara mbili zaidi kufikia tani 460,000 kutoka 295 za miaka saba iliyopita huku serikali ikijiwekea malengo sio tu ya kujitosheleza kwa sukari bali pia kuzalisha ziada ya kuuza nje ya nchi ili zipatikane fedha za kigeni kutatua changamoto za kijamii na kujenga miundo mbinu ya kiuchumi.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI