Header Ads Widget

VIONGOZI WA DUNIA WAWASILI KUMZIKA PAPA FRANCIS

 

Maelfu ya waombolezaji na makumi ya viongozi wa dunia wamefika tayari katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican, kwa ajili ya mazishi ya Papa Francis, aliyefariki Jumatatu ya Pasaka akiwa na umri wa miaka 88.

Ibada rasmi ya mazishi inatarajiwa kuanza saa 10:00 kwa saa za huko sawa na saa saba mchana kwa saa za Afrika Mashariki.

Katika hali isiyotarajiwa, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky,amewasili Roma asubuhi ya Jumamosi, baada ya kuwepo na wasiwasi kuwa huenda asingeweza kuhudhuria. Msemaji wake amethibitisha kuwasili kwake.

Rais wa Marekani, Donald Trump, pia amewasili, akiwa katika safari yake ya kwanza nje ya nchi tangu aanze muhula wake wa pili kama rais.

Mwandishi wa kipindi cha Today, Nick Robinson, kutoka Roma, anaeleza kuwa mazishi haya yameleta pamoja watu wenye nguvu zaidi duniani na wale waliotengwa zaidi, jambo linaloonyesha ushawishi mkubwa wa Papa Francis.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI