Arsenal wanapanga kutoa £55m kumchukua beki wa Barcelona, Jules Kounde, mwenye umri wa miaka 26. (The Sun)
Nottingham Forest inaweza kuendelea na mpango wa kumchukua kiungo wa Manchester City, James McAtee, mwenye umri wa miaka 22, hata kama wataendelea kuwa na wachezaji wa mbele, Callum Hudson-Odoi, mchezaji wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24, na Anthony Elanga wa Sweden mwenye umri wa miaka 22. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Uingereza, Jamie Vardy, mwenye umri wa miaka 38, huenda akajiunga na Wrexham wakati mkataba wake na Leicester City utakapomalizika msimu huu, ikiwa klabu hiyo ya Wales itapanda daraja kucheza Championship msimu ujao. (Talksport)
Manchester United itahamia kwa mchezaji wa RB Leipzig, Xavi Simons, mshambuliaji wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 22, ikiwa mpango wa kumchukua mshambuliaji wa Brazil wa Wolves, Matheus Cunha, mwenye umri wa miaka 25, utakwama. (Teamtalk)
Real Betis inajiandaa kutoa ofa ya mkopo wa msimu mzima kwa Manchester United ili kuendelea na mkataba wa kiungo wa Brazil, Antony, mwenye umri wa miaka 25. (Telegraph)
Chelsea inazungumza na wawakilishi wa winga wa Uingereza wa Borussia Dortmund, Jamie Gittens, mwenye umri wa miaka 20, kwa ajili ya uhamisho wa €50-60m (£42-52m). (Sky Germany)
Chelsea pia ina imani kwamba wataweza kumsajili mshambuliaji wa Uingereza wa Ipswich Town, Liam Delap, mwenye umri wa miaka 22, kabla ya Manchester United. (GiveMesport)
Strasbourg imefikia makubaliano ya kumbakisha klabuni kocha wa Uingereza, Liam Rosenior, mwenye umri wa miaka 40, licha ya kuvutiwa na klabu za Ligi Kuu England. (Athletic)
Manchester United inakutana na upinzani kutoka kwa mabingwa wa Ufaransa, Paris St-Germain, kwa ajili ya kiungo wa Napoli, Stanislav Lobotka, mwenye thamani ya £40m, lakini Barcelona pia inavutiwa naye. (Tuttomercato)
Kipa wa Uswisi anayechezea Borussia Dortmund, Gregor Kobel, mwenye umri wa miaka 27, huenda akaondoka klabuni hapo msimu huu kutokana na kuvutiwa na vilabu vya Chelsea na Newcastle United. (Footmercato)
Kipa wa Chelsea, Djordje Petrovic, mwenye umri wa miaka 25, anahitajika na Bayer Leverkusen kufuatia kiwango kizuri alichokionyesha akiwa kwa mkopo katika klabu ya Strasbourg msimu huu. (Kicker)
Beki wa Barcelona, Andreas Christensen, mwenye umri wa miaka 29, anataka kubaki klabuni hapo na kupigania nafasi yake badala ya kuhama msimu huu, licha ya mkataba wake kumalizika mwaka 2026. (AS)
Mshambuliaji wa Serbia, Dusan Vlahovic, mwenye umri wa miaka 25, mshambuliaji wa Uturuki, Kenan Yildiz, mwenye umri wa miaka 19, na mchezaji wa Italia, Andrea Cambiaso, mwenye umri wa miaka 25, ambaye anaivutiwa Manchester City, huenda wakalazimika kuondoka Juventus ikiwa klabu hiyo haitafanikiwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. (Calciomercato)
Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Nicolas Tié, aliyetumia muda wake katika timu ,a vijana za Chelsea, ameacha soka akiwa na umri wa miaka 24 ili kujiunga na jeshi la Ufaransa. (Ouest-France)
0 Comments