Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima App Dodoma
MTENDAJI Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, amesema uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania unatarajiwa kufanyika Jumamosi, Aprili 5, 2025, jijini Dodoma.
Jengo hilo ni kubwa zaidi barani Afrika na la sita kwa ukubwa duniani, likiwa na mita za mraba 63,244. Prof. Gabriel
Akiongea na waandishiwa habari leo Mtendaji mkuu huyo amefafanua kuwa mradi huu umejengwa kwa asilimia 100 kwa fedha za ndani, ukiwa na gharama ya Shilingi bilioni 129.7 huku Wageni wapatao 2,500 wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
0 Comments