Header Ads Widget

UVCCM WARIDHISHWA NA MRADI WA MAJI SIMIYU.

 

MWENYEKITI wa UVCCM Taifa (MCC), Mohamed Kawaida (wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wa serikali wakikagua ujenzi wa Tanki la Maji Somanda.


Na Costantine Mathias, Simiyu.


MWENYEKITI wa UVCCM Taifa (MCC), Mohamed Kawaida ameipongeaza serikali kwa kutekeleza Mradi wa Maji kutoka Ziwa Viktoria unaotekelezwa Mkoani Simiyu kwa gharama ya shilingi Bil.440 wenye lengo la kutatua kero ya Maji Mkoani humo.


Kawaida amesema kuwa ameridhishwa na Utekelezaji wa Ilani ya CCM na kwamba kazi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassani ni kutoa fedha za miradi ya Maendeleo huku viongozi wengine wakiwemo wakuu wa Mikoa na wilaya wanapaswa kuzisimamia ipasavyo.


Ameyasema hayo leo kwenye ziara ya kikazii Mkoani humo yenye lengo la kukagua Uhai wa Chama na Jumuiya zake, kuhamasisha vijana wajitokeze kwenye Uchaguzi Mkuu, kupiga kura, kuwania nafasi za Ubunge na Udiwani pamoja na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.


Amesema mwaka 2020, CCM ilipita kuomba kura Kwa wananchi na kuahidi kutekeleza miradi ya kimaendeleo pamoja kutatua kero za Wananchi ikiwemo kutekeleza Mradi huo wa Maji kutoka Ziwa Viktoria.


"Kazi ya Rais ni kutoa fedha, Wakuu wa mikoa na wilaya ni kusimamia miradi hii...nimeridhika mno na Utekelezaji wa Mradi huu ambao dhamira yake ni kutatua kero ya wananchi, niwaombe wataalamu wanaotekeleza Mradi huu watimize Malengo ya Rais Samia ili wafikie dhumini la Rais na Wananchi walindw miundombinu ya Maji" amesema.


Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amewataka vijana kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mpigakura pia wajitokeze kupiga kura na kuwania nafasi za uongozi.



Awali Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi amesema kuwa mradi wa huo wa Maji kutoka Ziwa Viktoria unatekelezwa kwa gharama ya shilingi Bil 440.


Amesema kuwa Rais Dk.Samia ameleta fedha ili kuhakikisha Mradi wa kimkakati unajengwa ambao utaanzia wilaya ya Busega na kusambaza kwenda Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu.


Amesema upatikanaji wa Maji katika Mkoa huo umefikia asilimia 79 na kwamba huko nyuma Mkoa wa Simiyu haukuwa na Maji ya uhakika kutokana na ardhi kuwa na magadi mengi 


Akisoma taarifa ya Mradi huo Meneja wa Baruwasa Mhandisi Msalika Masatu amesema wamejenga matenki 7 yenye uwezo wa kuhifadhia maji lita mil 39.5


Amesema Utekelezaji wa Mradi huo umefikia asilimia 23 ambapo wameeanza kulaza mabomba na pia Mradi utatochea Uchumi na ikiwemo kuongezeka kwa Viwanda.


Naye Rosemary Ng'hwani amesema wanafurahia kupata Mradi wa Maji ambao utawatua ndoo kichwani akina mama.


Mwisho.














Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI