Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC Imewaonya mawakala wa vyama vya siasa watakaoingilia majukumu ya waandikishaji watakaofanyakazi ya kuboresha daftari la mpiga kura awamu ya pili,zoezi linalotarajia kuanza Mei mosi hadi mei 7 mwaka huu katika mikoa 15 ya awali ukiwemo mkoa wa Njombe.
Katika Mafunzo kwa waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki katika daftari la kudumu la mpiga kura Jimbo la Njombe mjini Ofisa mwandikishaji jimbo hilo Samson Medda amesema kwa mujibu wa sheria mawakala hao wanaruhusiwa kuwepo katika vituo vya uandikishaji lakini sio kuingilia Majukumu ya waandikishaji kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria na kanuni za uchaguzi.
Awali waandikishaji hao wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki wamekula kiapo cha kutunza siri katika mchakato wa uandikishaji.
Mafunzo hayo yanatajwa kwenda kuwasaidia waandikishaji kutekeleza zoezi hilo kwa weledi ambapo baadhi yao akiwemo Happines Mwaituka na Christian Nyengela wanasema wanaamini watafanya vyema zoezi hilo baada ya mafunzo hayo.
Zoezi hilo linalokuja kwa awamu ya pili litatoa fursa ya kujiandikisha na kuboresha taarifa kwa wananchi ambao hawakufanikiwa awamu ya kwanza ili waweze kupata haki ya kikatiba ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao na kwa jimbo la Njombe mjini jumla ya vituo 45 vitatumika katika uboreshaji wa daftari hilo.
0 Comments