Header Ads Widget

TANAPA YAKUTANA NA WADAU ZANZIBAR KUJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI


Na. Jacob Kasiri - Zanzibar.

Timu ya Wataalamu wa Uhifadhi na Utalii kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wanaoshiriki Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar (ZITF) imekutana na wadau wa utalii na usafirishaji visiwani Zanzibar leo Januari 06, 2026 ili kubadilisha uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja kwa mwaka 2026.

Katika ziara hiyo ijulikanayo kama “door to door”, TANAPA walikutana na makampuni ya usafirishaji wa anga ya Auric Air Safari na Flightlink pamoja na Jumuiya ya Watembezaji na Waongoza Watalii Zanzibar (ZATO) lengo likiwa kujenga uhusiano, kufikia maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za Auric air Safari pamoja na Flightlink.

Aidha katika mazungumzo ya pamoja kati ya “TANAPA na ZATO”, Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Mashariki ACC John Nyamhanga, aliwasihi wadau kutoka Zanzibar kuwekeza ndani ya Hifadhi za Taifa Tanzania.



Naye, Bi. Hajla Saleh ambaye ni Meneja wa Kituo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume na mdau kuntu wa kampuni ya usafirishaji ya Auric Air, alieleza namna bora ya kuirisha safari za kutoka Zanzibar kwenda katika Hifadhi za Taifa Mikumi na Nyerere.

Ziara hizi za kukutana na wadau mbalimbali katika sekta ya utalii na usafirishaji ni katika kuimarisha ushirikiano, kujifunza na ni mkakati wa TANAPA kupata mrejesho wa namna bora ya kuboresha huduma  zake katika viwanja vya ndege na mazao ya utalii.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI