Header Ads Widget

ACT WAZALENDO YAPOKEA WANACHAMA 25 KUTOKA CCM KOJANI PEMBA

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman amepokea wanachama wapya 25  waliojiunga na Chama hicho kutoka Chama cha Mapinduzi CCM   Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Pemba.

Vijana hao wamejiunga leo 28 April 2025  katika mkutano wa hadhara unaoendelea muda huu katika viwanja vya Uwondwe Jimbo la Mtambwe.

Awali akiwakabiribisha vijana hao Mwenyekiti Mkoa wa Wete Juma Khamis Ali amesema vijana hao wamechoshwa na madhila ya CCM ambayo wamekua wakifanyiwa kila siku.

Amesema kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo vijana hao wataongeza nguvu ya kusimamia ushindi mkubwa wa Chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Awali vijana hao wamesema  maamuzi ya kujiunga Kwao na Chama cha ACT Wazalendo yametokana na madhila mbali mbali ambao wamekua wakipitia.

Abdalla Juma Faki amesema awali waliendelea kubaki CCM wakipewa ahadi tele zikiwemo za kupewa ajira lakini hadi leo hakuna aliefanikiwa katika wao.

"Walijenga maskani kwetu Kojani wakatufanya sisi ni watu wasiojitambua lakini sasa tumeamua kuunganisha nguvu zetu pamoja kukifanya Chama cha ACT Wazalendo kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Maimuna Makame Issa amesema alibaki CCM akipewa ahadi tele zikiwemo za mikopo ya Serikali iliolenga kuwainua wanawake kiuchumi lakini hawana walichopewa.

"Ni bora tubaki huku na wenzetu tupambanie Nchi yetu kuendelea kubaki CCM ni kupoteza muda na nguvu kwa watu wasiojali" alisema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI