Na Shomari Binda-Musoma
UTEKELEZAJI wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 kwenye Jimbo la Tarime Vijijini umempa uhakika mbunge wa jimbo hilo Mwita Waitara kurejea bungeni kwenye uchaguzi wa 2025.
Kauli hiyo ameitoa leo aprili 11 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti Kuu ya Serikali kwenye Kikao cha 4 cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12.
Akianza kutoa mchango wake ameishukuru serikali ya awamu ya 6 chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi kwenye jimbo hilo kwaajili ya utekelezaji wa miradi ikiwemo ya elimu.
Mbunge huyo amesema tangu mwaka 2021 majengo ya madarasa 376,yenye thamani ya zaidi ya bilioni 7 yamejengwa na shule mpya 19 zimejengwa,madawati,viti pamoja na meza.
Amesema ujenzi wa madarasa na shule hizo imewezesha wanafunzi kupata elimu ya uhakika na hakuna mzazi aliyechangishwa fedha.
Waitara amesema licha ya sekta ya elimu ndani ya jimbo la Tarime Vijijini wakandarasi wapo kazini kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya maji,afya na barabara na kuomba kasi iongezeke kwenye eneo hilo ili kucĥochea kasi ya maendele.
Waitara ameupongeza pia mgodi wa Barrick North Mara kwa kitoa fedha za CSR zaidi ya bilioni 6 ambazo zìpo kwenye akaunti za vijiji kwaajili ya utekelezajj wa miradi.
Amesema uzoefu wa miaka 10 alionao bungeni umemuwezesha kujua njia mbalimbali za kufatilia fedha za utekelezaji wa miradi na kuwezesha jimbo kusonga mbele kimaendeleo.
" Nimekuwa na uzoefu ndani ya bunge hili kwa vipindi viwili kwenye majimbo mawili tofauti na mikoa tofauti na tumekubaliana watanirejesha tena hapa bungeni.
"Utekelezaji mkubwa wa ilani umetekelezwa kuanzia sekta ya elimu kwa Dkt.Samia kutupatia fedha nyingi za miradi na hadi sasa wakandarasi wapo maeneo ya miradi wakiendelea na kazi",amesema.
Katika mchango wake Waitara pia amewataka wananchi wa mikoa ya kusini kuacha kudanganywa na wale aliowata wanaharakati wa kisiasa.
Ameongeza kuwa watanzania watambue seriki ya Chama cha Mapinduzi imefanya kazi kubwa ya maendeleo na kudai hakuna upinzani.
Amesema chama pekee chenye watu makini na kuweza kuliongoza taifa ni Chama cha Mapinduzi na kudai uchaguzi utafanyika na kushinda kwa kishindo.
0 Comments