Na Shomari Binda-Musoma
WAANDAJI wa tuzo za Mwanamke Gala mkoa wa Mara Fugo Company Limited wametoa tuzo kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi kwa kutambua mchango wao kwa taifa.
Licha ya viongozi hao kukabidhiwa tuzo hizo wanawake waliofanya vizuri kwa sekta mbalimbali Wilaya ya Musoma pia wamekabidhiwa tuzo.
Akipokea tuzo hizo zilizotolewa usiku wa jana mjini hapa kwa niaba ya viongozi hao,Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amesema waandaaji wamefanya jambo kubwa na yupo tayari kuwaunga mkono.
Amesema tukio ni kubwa na limeandaliwa kwa ubora na kudai ni heshima kutambua mchango wa viongozi na kuwapa tuzo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mara ambaye alikuwa amealikwa kama mgeni rasmi Chikoka amesema ofisi ya mkuu wa mkoa na ofisi yake wapo tayari kuwasaidia wanawake wanapokuwa wana matukio yao yenye mchango kwa jamii.
Amesema tuzo hizo zitatoa ari kwa wanawake wengine kujituma kwenye kazi zao zikiwemo za ujasiliamali ili kuwainua kiuchumi.
Chikoka amesema ili kuwaunga mkono atahakikisha wanawake wanapewa kipaumbele katika kupata mikopo isiyo na riba kutoka kwenye halmashauri ili mji wa Musoma uendelee kuchangamka kwenye matukio.
Muandaji wa tuzo za Mwanamke Gala mkoa wa Mara Anifa Majura " mama Fugo" amesema wanatambua mchango wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuwainua wanawake na kuamua kumpa tuzo hiyo.
Amesema wataendelea kumsemea kwa mazuri aliyofanya huku wakimshukuru mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi kwa kuwapa ushirikiano..
Tuzo za Mwanamke Gala 2024 huu ni msimu wake wa pili kufanyika na wanawake waliofanya vizuri kwenye fani mbalimbali wamekabidhiwa tuzo huku burudani zikiongozwa na msanii Christian Bella
0 Comments