Header Ads Widget

MBIO ZA KIUTALII KUKUZA UCHUMI NA KUIMALISHA UZAZI SALAMA KWA MAMA WAJAWAZITO.

 


Mtaribu wa Huduma ya Afya ya Uzazi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bertha Yohana,

Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro One Sports Promotion Limited
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi akiwa katikati pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro One Sports Promotion Limiteda wa kwanza kushoto wakizundua jezi zitakazotumika katika mbio Lake zone International Tourism Marathon Mkoani Mwanza


NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA.


Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Amina Makilagi ameeleza kuwa mbio za kiutalii zitakazofanyika Jijini hapa zitakuza uchumi na kuongeza fursa mbalimbali lengo likiwa ni kukusanya fedha ili kuwagusa wanawake  wajawazito ili kuwawezesha na kuwasaidia kununua vifaa tiba Kwa ajili kuimalisha uzazi salama Kwa wanawake wajawazito na watoto Kwa ujumla.




Akizungumza na waandishi wa habari, wadau wa utalii pamoja na baadhi ya wanariadha katika uzinduzi wa Lake zone International Tourism Marathon 2025 ameeleza kuwa mbio hizo mbali na kutembelea na kutangaza vivutio vya utalii ili kukuza uchumi Kwa Kanda ya Ziwa zitamsadia mjamzito kuimalisha mfumo mzima na kupata Mtoto aliye salama, uzazi salama na kutengeneza Taifa lililosalama.




Makilagi ameeleza kuwa sekta ya utalii inamchango kubwa katika kuongeza Pato la Taifa Kwa asilimia 17 na kutoa ajira Kwa mtu moja moja zaidi ya watanzania Mil 1.6 wameweza kunufaika.



"Kama alivyosema Mganga Mkuu wa Mkoa kwamba vifo vya wanawake na watoto Kwa Mkoa wetu wa Mwanza kupitia mbio hizo zinaenda kukoma kukoma ambapo ni dhamira ya Rais wetu wa jamhuri ya Muungani wa Tanzania" Alisema Makilagi.



 Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro One Sports Promotion Limited, Mohamed Khatibu ameeleza kuwa mbio hizo zinatarajiwa kuanza juni 27 Hadi 29 Jijini hapa lengo likiwa ni kutangaza vivutio vya kiutalii na fursa za kiuwekezaji zinazopatikana katika kuelekea katika tamasha la kiutamaduni la Kanda ya ziwa litakalofanyika Mkoani Simiyu



"Madhumuni makubwa ya mbio hizi ni kutangaza vivutio vya kiutalii na fursa za kiuwekezaji zinazopatikana katika Jiji la mwanza ili kukuza uchumi wa kanda ya ziwa na Taifa kwaujumla", Alisema Khatibu



Aidha,Khatibu ameeleza kuwa kila uwekezaji wa kiuchumi unahitaji utulivu wa nchi na amani ya watu wake, hivyo watatumia mbio hizo kuhamasisha wananchi wote kujitokeza kujiandikisha na kushiriki uchanguzi Mkuu Oktoba 2025 kwa amani.



Kwa upande wake Msimamizi Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)Ofisi ya Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua alisema watatumia michezo kama mkakati wa kutangaza utalii nchini kutokana na michezo kuwa uchumi,afya na utalii.



"Michezo inaleta  watu kutoka sehemu mbalimbali hivyo mkoa utapata ongezeko la uchumi,watu watafanya mazoezi afya zitaimarika na watapata fursa ya kutembelea vivutio na mazao ya utalii",



Naye Mtaribu wa Huduma ya Afya ya Uzazi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bertha Yohana, alisema mbio hizo ni fursa kubwa kwani itawasaidia kuendelea kutoa elimu kwa wajawazito ambayo itasaidia kupunguza vifo.

Bertha ameeleza kuwa katika mbio hizo wajawazito watashiriki kwakufanya mazoezi mepesi ikiwemo kutembea kwa dakika 20 hadi nusu saa hatua itakayosaidia kuimarisha afya zao.

"Kuna faida nyingi za kufanya mazoezi kwa wajawazito,ikiwemo kupunguza uzito,kusaidia mzunguko wa damu kwenda vizuri pamoja na kupata usingizi mzuri", Alisema Yohana

Katika mbio hizo za lake zone International Tourism Marathon 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda ndio atakuwa Balozi wake.



SIMULIZI NZURI CHINI ⬇️ ⬇️ 👇 


Je, ni kweli wanawake wasomi huchelewa kuolewa?

Nakumbuka kuna mtu mmoja katika mtandao wa X, zamani Twitter aliuliza kwanini mahusiano au ndoa za watu ambao hawajasoma zinadamu kuliko za wale ambao wana elimu kubwa?.

Swali hilo lilikuwa likigusa maisha yangu kutokana nilikuwa mwanamke ambaye kila mara nilijikuta katika mahusiano mapya, suala la elimu yangu lilifanya wanaume kuugopa kunio. 

Naitwa Shami, nina shahada mbili ukapande IT, nimeajiriwa katika kampuni fulani nikiwa kama Mkuu wa Kitengo, nimefanya kazi hii kwa zaidi ya miaka 10 na nimeweza kutengeneza maisha yangu vizuri tu. 

Naweza kusema katika maisha yangu upande wa elimu na kazi sijapitia changamoto nyingi kama zile nilizopitia upande wa mahusiano, huku nimezungushwa sana hadi nafikisha umri wa miaka 40 nilikuwa sijaolewa. 

Kila mwanaume niliyekuwa naye katika mahusiano nikimwambia umefika wakati sasa tufunge ndoa au akajitambulishe kwa wazazi wangu alikuwa anatafuta  sababu ya kukimbia. Baadhi ya watu wanasema wanaume wengi wanaogopa kuoa wanawake wasomi kutokana wanaona ni vigumu kuwasimamia kitu ambacho naona sio kweli. 

Mimi kama mke nina wajibu wa kumtii na kumjali mume wangu, siwezi kuwa na kiburi au kufanya jeuri kisa nimesoma au nimemzidi elimu, hapana!. Hata mume wangu wa sasa ni shahidi katika hilo na mwenyewe  anasema hakutarajia kama ni mtu wa hivyo kwani hata mwanzo tulivyofunga ndoa alikuwa na aina fulani ya wasiwasi.

Nakumbuka baada ya mahusiano yangu kama ya nne kuvunjika, niliamua kutafuta njia mbadala, hiyo ni baada ya kuona nimefikisha miaka 38 bila kuolewa jambo ambalo lilifanya hata nyumbani kwetu kuanza kuniuliza maswali. 

Katika kutafuta wapenzi waaminifu katika mtandao, nilijikuta nimeingia kwenye wavuti ya Kiwanga Doctors, hapa nilipata kufahamu kuwa anaweza kuwasaidia wanawake kupata waume kwa muda mfupi tu. 

Hatimaye nilichukua namba yake na kuwasiliana naye mara moja, Kiwanga Doctors kutokea Migori, Kenya, aliniambia licha ya umri wangu wa miaka 38 nisiwe na hofu kwani nitapata mume tena mwenye viwango. 

Nilingojea kwa hamu kuona hilo likitimia katika maisha yangu maana ilifika hatua hadi naogopa kwenda nyumbani kusalimia kwa kuhisi wataanza kuniuliza kwanini hadi sasa sijaolewa. 

Jioni moja nikiwa natokea kazini niliita Uber ije inichukue, kufika yule dereva wa Uber alikuwa ni rafiki yangu wa miaka mingi ambaye tulikuwa tumeshibana kipindi tunasoma sekondari. 

Yule kaka alifurahi sana kukutana na mimi na kuniambia kuna wakati walitafuta mawasiliano yangu bila mafanikio, tulizungumza mengi na akanipeleka hadi nyumbani na kumuonyesha ninapoishi.  Tulibadilishana namba za simu na akaniahidi kwamba wikiendi atakuja kunitembelea. 

Wikiendi iliyofuatia alikuja nyumbani tukakaa na kuzungumza, alinieleza kwamba kuna wakati alioa ila alikuja kuachana na mkewe miaka mitatu iliyopita na sasa hana mtu. 

Sikutaka kujirahisisha kwake, tuliendelea kuwasiliana na kutembeleana hadi pale yeye mwenyewe aliponitamkia kuwa ananipenda na anataka kunioa. 

Nilifurahi sana kusikia hivyo, mara moja tulianza michakato ya kutambulishana kwa wazazi kwa pande zote mbili na hatimaye tulifunga ndoa na sasa tumejaliwa kupata mtoto mmoja. 

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba  +255 763 926 750 au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI