Shemsa Mussa -Matukio daima Kagera.
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoani Kagera imetoa tahadhari na umakini kwa madereva wote wanaotumia Barabara hasa katika kipindi hiki Cha matengenezo yanayoendelea katika maeneo tofauti tofauti ya Mkoa huo.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera, Mhandisi Ntuli Mwaikokesya, ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Mwandishi wetu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na usalama barabarani.
Mhandisi Mwaikokesya amewasihi madereva kuzingatia alama na sheria za barabarani na kufuata maelekezo yanayotolewa,Pia Ameeleza kukerwa na tabia ya baadhi ya madereva wanaoshindwa kufuata taratibu za kisheria kwa maeneo yasiyoruhusiwa kupita.
Aidha,Mwaikokesya Amefafanua kuwa maeneo ambayo yamewekwa kisheria kwa ajili ya ustawi wa barabara ni muhimu kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara, hivyo ni marufuku kufanya shughuli nyingine kama biashara katika maeneo hayo.
Mwaikokesya amesisitiza kuwa, kwa mujibu wa sheria ya barabara, hairuhusiwi mtu kufanya shughuli yoyote ndani ya hifadhi ya barabara,Ameonya kuwa, endapo ajali itatokea, wafanyabiashara walioko pembezoni mwa barabara hawatakuwa salama.
"Ni muhimu kwa Wananchi kutokaa kwenye hifadhi ya barabara, ndiyo maana kuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli zote za kiuchumi Barabara sio salama kukaa lolote linaweza kutokea,amesema Mwaikokesya"
Mhandisi Mwaikokesya ametoa ahadi kwa Wananchi wa Kagera kuwa wao kama TANROADS wanafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha Barabara zote zinapitika na matengenezo yanakamilika kwa wakati.
Amesema endapo hata mvua zikinyesha haziwezi kuwa sababu ya kukatika kwa mawasiliano ya muda mrefu kwani wataalam kuhakikisha barabara zinabaki salama ndani ya muda wa Saa 48.
0 Comments