Na Shemsa Mussa -Matukio daima Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema huwezi kuwa na chanzo kimoja cha Mapato ukapata maisha bora na kwamba lazima uwe na sehemu tofauti tofauti za kuchuma.
Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazazi na watahiniwa wa mitihani ya kidato cha sita katika shule za sekondari Kemeboz na Kaizirege zilizopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.
Andengenye amesema, ujuzi wa jambo lolote katika mazingira anayoishi binadamu aliyejaaliwa nguvu unasaidia kuboresha maisha na sio kutegemea ajira pekee.
Amesema,yapo maeneo ambayo yameandaliwa na Serikali kwa ajiri ya kumlahisishia mwananchi kwenda kujifunza na kujipatia ujuzi utakaomwezesha kuanzisha uzalishaji na kupata kipato na maisha anayotamani kuwa nayo.
"Maeneo kama, vyuo vya kati,vyuo vikuu, jeshi la kujenga Taifa vinauwezo wa kufundisha ufugaji,ufundi uashi,umeme na kilimo haya machache yatasaidia sana kwa vijana wetu" alisema Andengenye
Aliongeza kwa vijana ambao watahitimu masomo ya kidato cha sita ni muda sasa wa kuanza kufikiri jinsi ya kuwa na ujuzi mara tu wamalizapo masomo yao.
Askofu mstaafu wa kanisa la agrikani mjini Bukoba Elisha Bililiza amesema watahimiwa ambao wanategemewa sasa kumaliza masomo yao na baada ya miaka miwili shuleni, elimu hiyo ifanikishe katika malengo yao.
Alisema,kufanikisha malengo yao sio ajira pekee bali hata akili waliyonayo iwaongoze kwenye maisha ili yaweze kuwa bora zaidi
na kusema kuwa akili ndio inayoongoza kufikiri yaliyoko mbele zaidi katika maisha ya uchumi na sio elimu pekee ya darasani ambayo wamepatiwa kwa miaka miwili.
Awali akisoma risala Mkuu wa shule hizo Mwl Kisha Ilamulira amesema ujuzi na ubunifu ndio Moja ya mafanikio ya kuwepo na shule hizo kwani Mkurugenzi wa shule aliweza kufanya kazi kwa juhudi na maarifa,amesema ipo Imani hata wahitimu wa shule hizo wataweza kwenda kuanzisha ubunifu mbalimbali ikiwa ni baada ya kumaliza elimu zao za kati na juu.
"Endapo watatafsiri maoni ya Mkurugenzi wetu, itawajenga hata wao kuwa na ujuzi wa aina yoyote ambao wataanzisha miradi na kujiajiri na jitihada walizozipata darasani ndizo ziwafanyie uthubutu wa mafanikio"alisema Ilamulira
Julma ya watahiniwa 248 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza kidato Cha sita mnamo 05may 2025 ,ikiwa wasichana ni 125 na wavulana ni 123.
0 Comments