Mdau wa Michezo na Mwanamichezo nchini Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo- Malya, Dkt. Jonas Tiboroha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Michezo BMT, akikabidhi zawadi ya kikombe cha ubingwa wa DSSL2025 kwa Nahodha wa TRA SC , April 5,2025
Na Andrew Chale, Matukio Daima App Dar.
TIMU ya Mpira wa miguu ya Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ya TRA SC imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa kombe la Mashindano ya Wafanyakazi Dar Es Salaam 'Dar Es Salaam Staff Sports League' (DSSL) kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) waliokubali kichapo cha bao moja bila.
Mchezo huo wa fainali wa aina yake umechezwa katika uwanja wa TRA Kurasini, Aprili 5, 2025 ulishuhudiwa na shamrashamra na shangwe mbalimbali kwa mashabiki wa timu zote mbili ulikuwa wa kuvutia licha ya mvua iliyokuwa ikinyesha dakika 45 za kwanza za mchezo huo,
Hata hivyo TRA SC walifanikiwa kupata bao kipindi cha pili, na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo, na kuwafanya kuwa mabingwa wapya wa kihistoria kwa kutwaa mfululizo, wakifanya hivyo mwaka jana 2024, na mwaka huu 2025.
 |
Mdau wa Michezo na Mwanamichezo nchini Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo- Malya, Dkt. Jonas Tiboroha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Michezo BMT, akisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili TRA wenye jezi ya njano na nyeusi (chini) na juu timu ya IFM wenye jezi za bluu katika mchezo wafainali ya DSSL2025 , April 5,2025 |
TRA pia wameweza kuweka rekodi ya kipekee kwa upande wa timu ya Wanawake ya mchezo wa Netball waliweza kutwaa ubingwa dhidi ya Timu ya Wanawake ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), na kufanya TRA kuwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo.
Awali akikabidhi zawadi za ushindi, Mdau wa Michezo na Mwanamichezo nchini Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo- Malya, Dkt. Jonas Tiboroha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Michezo BMT, alipongeza vipaji vya wachezaji wa timu zote huku akiomba maafisa Uajili kuendelea kuwekeza zaidi michezoni kwani inasaidia Wafanyakazi kuwa vyema kiafya na ufanisi kazini.
"Niwapongeze viongozi wa timu zote bahati nzuri mpo hapa.
Michezo inasaidia ufanisi, inapunguza hata bajeti ya matibabu, tuendelee kuwekeza kwenye michezo na tuangalie namna ya kuweka sawa Miundombinu ya michezo." Amesema Dkt Toboroha na kuipongeza TRA kwa ujenzi wa uwanja huo wa kurasini hali inayowapa ufanisi mkubwa kwa kushinda makombe katika michuano mbalimbali ikiwemo SHIMUTA na mingine mingi ya Wafanyakazi nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ligi hiyo, Japhari Saidi Mtoro amezipongeza timu zote kwa hatua waliofikia, huku akiahidi msimu ujao mambo makubwa.
"Mashindano ya wafanyakazi lazima yalindwe kwa nguvu na wivu mkubwa, hivyo ni muhimu kuwekeza katika mifumo itakayozuia mtu yeyote asiye na sifa kushiriki mashindano hayo.
Akifafanua zaidi Mwenyekiti amesema kuanzia msimu unaokuja wataweka mfumo wa biometric utakaotumika kuwasajili na kuwatambua wachezaji kwa sura zao na alama za vidole.
Mashindano hayo yalishirikisha timu 14, zilizocheza mfumo wa Ligi, kila wiki ilikujenga Afya ya Watumishi wachezaji maofisini lakini pia kujiandaa na michezo mbalimbali pahala pa kazi.
 |
Mchezaji wa mpira wa Netball wa TRA akina amemiliki mpira dhidi ya mchezaji wa MSD |
 |
Wachezaji wa IFM |
 |
Wachezaji wa IFM wakipokea zawadi ya Medali ya mshindi wa Pili |
 |
Wachezaji wa TRA mchezo wa Netball wakipokea zawadi ya Medali na kikombe wakiibuka washindi kwa mwaka wa pili mfululizo wa michezo hiyo upande wa Netball |
 |
Mchezaji bora wa TRA SC akipokea zawadi kutokakwa Mwenyekiti wa DSSL, Japhari Saidi Mtoro |
 |
Mchezaji wa IFM akipokea zawadi ya mfungaji bora |
 |
Golikipa wa IFM akipokea zawadi ya golikipa Bora DSSL 2025 |
 |
Wachezaji wa IFM |
 |
Kiongozi wa Michezo TRA |
 |
Wachezaji na Staff wa TRA wakiwa na bango la kuhamasisha kuhakikisha stempu kidijitali |
 |
Maafisa w TRA wakiselebuka baada ya ushindi wa kombe la DSSL 2025 |
 |
Mashabiki wakifurahia mchezo huo wa fainali ya DSSL 2025 |
 |
Wachezaji wa TRA wakifurahia ushindi |
 |
fainali ya mchezo wa Netball baina ya TRA na MSD |
0 Comments