Katika kuunga Mkono juhudi za Serikali kwenye kuinua michezo nchini wadau mbalimbali wamejitokeza katika kuinua vipaji vya vijana katika mchezo wa soka wa Samia Cup 2025 Wilaya ya Kigamboni wilayani Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa hatua ya nusu Fainali wa mashindano ya Samia Cup Wilaya ya Kigamboni Mdhamini Mkuu wa Mashindano hayo Dotto Rweikiza amesema lengo la mashindano hayo ni kuunganisha nguvu ya pamoja na kuisaidia Serikali katika kuibua vipaji vya michezo nchini kwani michezo ni ajira.
Kwa upande wake mratibu wa Mashindano hayo Omari Rajab amesema wamealika maskauti kutoka katika vilabu mbalimbali nchini kwa ajili ya kujionea na kuchukua vipaji vipya katika mashindano hayo huku akitaja zawadi za washindi.
Mchezo huo wa nusu fainali umepigwa katika Uwanja wa Mji Mwema Kigamboni umeshirikisha timu za Wahenga Fc na Tandika Fc waliokubali kufungwa magoli 2-1.
Mashindano hayo yanatarajia kufikia tamati katika mchezo wa fainali kati ya Wahenga Fc na Dream Team utakaopigwa Aprili 5 mwaka huu wakati mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu utachezwa Aprili 4 kati ya Mbutu Fc na Tandika Fc.
0 Comments