Header Ads Widget

RC MTAMBI APOKEA MADAWATI,VITI NA MEZA KUTOKA MGODI WA BARRICK NORTH MARA-MBUNGE WAITARA ATOA PONGEZI


Na Shomari Binda--Matukio Daima

MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amepokea awamu nyingine ya madawati, viti na meza vinavyotengenezwa na mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya wilaya ya Tarime.

Mtambi amepokea madawati 310 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi, viti na meza 295 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari.

Madawati, meza na viti hivyo vinatengenezwa kupitia mpango wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamiii (CSR) wa mgodi  huo ambao unaoendeshwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals yamekabidhiwa jana aprili 15,2025

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo mkuu huyo wa mkoa amesema amefarijika kupokea madawati hayo na kudai ameyakagua na kuona ni mazuri na yana ubora unaotakiwa.


Mbele ya wahudhuriaji walioshuhudia tukio hilo lililofanyika kwenye shule ya sekondari Ingwe iliyopo katika mji mdogo wa Nyamongo amesema mgodi huo unastahili pongezi kwenye uwajibikaji wake.

Amesema hadi mradi huo utakapokamilika utaghalimu kiasi cha shilingi milioni 898 fedha ambazo ni nyingi na zinakwenda kusaidia jamii eneo la wanafunzi kupata elimu.

" Nichukue nafasi hii kuupongeza mgodi wa Barrick North Mara kwa kuendelea kutekeleza masuala mbalimbali ya kuhudumia jamii.

" Madawati,viti pamoja na meza mlizoxitoa zinakwenda kusaidia kwenye shule zetu za msingi na sekondari hongereni sana kwa kazi nzuri" amesema.


Akizungumza katika hafla hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara Apolinary Lyambiko amesema utengenezaji wa madawati hayo ni moja wa miradi 101 ambayo utekelezaji wake unaendelea katika Halmashauri ya Wiaya ya Tarime kwa gharama ya shilingi zaidi ya bilioni 9 zilizotolewa na mgodi huo kupitia mpango wake wa CSR.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara amesema kampuni ya Barrick inafanya kazi nzuri katika kuwezesha na kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika jimbo hilo.


Amesema msimamo wake ni kuendelea kuunga mkono uwekezaji wa kampuni ya Barrick katika mgodi huo kwani una faida kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

“Huyu ni mwekezaji anafanya shughuli zake na anafanya mambo makubwa kuwezesha makundi mbalimbali ya wananchi na shughuli za kijamii lazima tuwaunge mkono.

" Mgodi umetoa mabilioni ya fedha yakiwemo ya ushuru wa huduma kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime lakini pia gawio la mrabaha kwa vijiji vitano na mahusiano yamekuwa mazuri na wananchi wanaozunguka mgodi tofauti na miaka ya nyuma:,amesema

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI