Na Matukio Daima Media
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu, Moses Ambindwile, Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkurugenzi wa Kampuni ya Sheria ya Icon Law yenye makao yake mjini Iringa, ametoa wito kwa Watanzania wote kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura ili kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya taifa.
Akizungumza kupitia Matukio Daima TV, Wakili Ambindwile amesisitiza kuwa kushiriki uchaguzi ni wajibu wa kiraia na nafasi ya kuamua mustakabali wa taifa.
"Kura yako ni sauti yako. Usiruhusu wengine wakufanyie maamuzi," amesema wakili Ambindwile
Ameongeza zaidi kuwa faida za Kushiriki Uchaguzi ni nyingi na miongoni mwa hizo ni kama ifuatavyo:-
Kuwa Kuchagua viongozi bora kwa Kupitia kura yako, unawachagua wale wenye maono, uadilifu na dhamira ya kulitumikia taifa.
Pia alisema Kuimarisha demokrasia kwani Kadri wananchi wanavyoshiriki kwa wingi, ndivyo demokrasia inavyokuwa imara zaidi.
Aidha alisema Kuwawajibisha viongozi kwani Wanajua kuwa madaraka yao yanategemea ridhaa ya wananchi, hivyo hulazimika kutimiza wajibu wao.
Hata hivyo alitaja baadhi ya Madhara ya Kutoshiriki ambayo mwananchi atayapata kuwa ni pamoja na kupoteza nafasi ya mabadiliko kwa kuwa Kutoshiriki kwenye uchaguzi ni kuacha hatima ya nchi mikononi mwa wachache.
Wakili Ambindwile pia alisema Demokrasia kudumaa kutokana na Idadi ndogo ya wapiga kura husababisha uchaguzi usioakisi matakwa ya wengi,Kukosa haki ya kuhoji kwani bila kupiga kura, unakosa msingi wa kuwasema viongozi waliopo madarakani.
Moses Ambindwile aliwashauri vijana ,wazee, wanaume na wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi kama wapiga kura, akisisitiza kuwa:
"Vijana ni taifa la sasa na kesho, wanawake na wanaume ni nguzo ya maendeleo – kila sauti inahitajika."
“Kura moja inaweza kubadili historia ya taifa. Usione ni ndogo – ni silaha ya mabadiliko na ujenzi wa taifa bora.” Na kwamba UCHAGUZI NI NGUZO YA MAENDELEO – WANA IRINGA NA WATANZANIA, TUJITOKEZE KWA WINGI!
0 Comments