Header Ads Widget

MAKAMU WA RAIS DKT NCHIMBI AKUTANA NA BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA MHE BASHWADIP DEY



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazugumzo na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Bashwadip Dey, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 20 Februari 2026.

Mazungumzo hayo, yamelenga kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya India na Tanzania katika sekta mbalimbali za kimkakati. Mahusiano kati ya nchi hizi mbili yamejikita katika sekta ya Afya, Maji, Elimu,Biashara na Uwekezaji pamoja masuala ya Ulinzi na Usalama.

Tanzania na India zina mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyoanza baada ya Tanzania kupata uhuru ambapo India ilifungua Ubaozi wake mwaka 1961 na Tanzania kufungua Ubalozi wake nchini India mwaka 1962.

Mwaka 2023 mahusiano kati ya nchi hizi mbili yaliongezeka zaidi na kuwa mahusiano ya kimkakati kufuatia ziara rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoifanya nchini India.

India imekuwa na mchango mkubwa katika miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa na Serikali pamoja na kutoa mchango mkubwa katika sekta ya Afya ikiwemo utoaji wa huduma za afya nchini, mafunzo pamoja na Vifaa Tiba.  

India imekuwa mdau muhimu wa biashara nchini Tanzania ambapo hadi sasa inashika nafasi ya tatu duniani kwa kufanya biashara na Tanzania. Bidhaa ambazo Tanzania inauza zaidi nchini India ni pamoja na Korosho, karanga, mboga za jamii ya kunde, vito vya thamani na vito vya thamani, pamba; karafuu, chai, Ngozi, mbao na bidhaa za mbao.
 
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
20 Februari 2026
Dar es Salaam.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI