Jasmine Ng'umbi mjumbe kamati ya utekelezaji UVCCM wilaya ya Mufindi
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Ikumbukwe kuwa jumapili ya Matawi ni siku muhimu sana katika kalenda ya Wakristo duniani kote.
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji UVCCM wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Jasmine Ng'umbi anasema kuwa .
Hii ni siku ambayo huadhimisha kuingia kwa Yesu Kristo mjini Yerusalemu, akipokelewa kwa shangwe na watu waliokuwa wameshika matawi ya mitende, wakimlaki kama Mfalme wa Amani.
Kuwa tukio hili linaashiria mwanzo wa Wiki Takatifu inayoelekea kwenye mateso, kifo, na hatimaye ufufuko wa Bwana Yesu Kristo – kiini cha imani ya Kikristo.
Katika muktadha wa Jumapili ya Matawi, ni vyema kila mmoja wetu aitumie siku hii kwa kutafakari kwa kina.
Tafakari hii haipaswi kuwa ya kiroho tu, bali pia iwe ya kijamii na kimaendeleo.
Jasmine Ng'umbi anasema Kama Vijana wa Mufindi,wananchi na taifa kwa ujumla, tunayo nafasi ya kujiangalia upya katika namna tunavyoishi, tunavyoshirikiana, na jinsi tunavyoshiriki katika maendeleo ya jamii zetu.
Yesu alipoingia Yerusalemu, alileta ujumbe wa amani, unyenyekevu, na upendo.
Vivyo hivyo, sisi kama Vijana tunapaswa kutambua kuwa maendeleo hayawezi kufikiwa bila kuwa na moyo wa mshikamano, amani, na kushirikiana kwa dhati.
Jumapili hii itufundishe kuwa maendeleo si kazi ya mtu mmoja, bali ni jukumu la kila mmoja wetu.
Katika kutafakari maendeleo, tujiulize: tumefanya nini kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bora?
Tumechukua hatua gani kusaidia wakulima kupata mbegu bora, masoko, na maarifa ya kisasa?
Tumekuwa mstari wa mbeleje kupambana na changamoto kama upungufu wa huduma za afya, barabara, na maji safi? Hili ni jukumu letu sote – viongozi, wananchi, na wadau wa maendeleo kama mimi na wewe.
Anasema kuwa Mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan yanategemea uelewa wetu wa pamoja kuhusu wajibu wetu.
Jumapili hii ya Matawi iwe mwanzo wa kuamsha mioyo yetu kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
Kama Yesu alivyoingia Yerusalemu kwa lengo la kuleta wokovu, nasi tuingie katika maisha yetu ya kila siku tukiwa na nia ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii zetu.
Mwisho, nawatakia wakazi wote wa Vijana wote Mufindi na watanzania kwa ujumla heri ya Jumapili ya Matawi.
Iwe ni siku ya amani, tafakari, upendo, mshikamano, na nia mpya ya kujitoa kwa ajili ya ustawi wa kila mmoja wetu.
Tujikumbushe kuwa maendeleo ni matokeo ya juhudi za pamoja, maono ya pamoja, na imani kuwa kwa kushikamana, tunaweza kuyafikia.
#Kazi na Utu Tunasongambele Mbele
0 Comments