Header Ads Widget

NAWATAKIA HERI YA JUMAPILI YA MATAWI – AIDAN MLAWA, MDAU WA MAENDELEO KILOLO

NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

Ikumbukwe kuwa jumapili ya Matawi ni siku muhimu sana katika kalenda ya Wakristo duniani kote.

 Mdau wa maendeleo wilayani Kilolo mkoani Iringa Aidan Mlawa anasema kuwa hii ni  siku ambayo huadhimisha kuingia kwa Yesu Kristo mjini Yerusalemu, akipokelewa kwa shangwe na watu waliokuwa wameshika matawi ya mitende, wakimlaki kama Mfalme wa Amani. 

Tukio hili linaashiria mwanzo wa Wiki Takatifu inayoelekea kwenye mateso, kifo, na hatimaye ufufuko wa Bwana Yesu Kristo – kiini cha imani ya Kikristo.

Katika muktadha wa Jumapili ya Matawi, ni vyema kila mmoja wetu aitumie siku hii kwa kutafakari kwa kina.

 Tafakari hii haipaswi kuwa ya kiroho tu, bali pia iwe ya kijamii na kimaendeleo.

 Mlawa alisema Kama wananchi wa Kilolo na taifa kwa ujumla, tunayo nafasi ya kujiangalia upya katika namna tunavyoishi, tunavyoshirikiana, na jinsi tunavyoshiriki katika maendeleo ya jamii zetu.

Yesu alipoingia Yerusalemu, alileta ujumbe wa amani, unyenyekevu, na upendo.

 Vivyo hivyo, sisi kama watu wa Kilolo, tunapaswa kutambua kuwa maendeleo hayawezi kufikiwa bila kuwa na moyo wa mshikamano, amani, na kushirikiana kwa dhati.

 Jumapili hii itufundishe kuwa maendeleo si kazi ya mtu mmoja, bali ni jukumu la kila mmoja wetu.

Mlawa alisema katika kutafakari maendeleo, tujiulize: tumefanya nini kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bora? 

Tumechukua hatua gani kusaidia wakulima kupata mbegu bora, masoko, na maarifa ya kisasa? 

Tumekuwa mstari wa mbeleje kupambana na changamoto kama upungufu wa huduma za afya, barabara, na maji safi? Hili ni jukumu letu sote – viongozi, wananchi, na wadau wa maendeleo kama mimi na wewe.

Alisema kuwa Mafanikio ya Kilolo yanategemea uelewa wetu wa pamoja kuhusu wajibu wetu. 

Kwani jitihada kubwa chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan zimefanyika wilaya ya Kilolo imefunguka Kimaendeleo.

Jumapili hii ya Matawi iwe mwanzo wa kuamsha mioyo yetu kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo. 

Kama Yesu alivyoingia Yerusalemu kwa lengo la kuleta wokovu, nasi tuingie katika maisha yetu ya kila siku tukiwa na nia ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii zetu.

"Mwisho, nawatakia wakazi wote wa Kilolo na watanzania kwa ujumla heri ya Jumapili ya Matawi Iwe ni siku ya amani, tafakari, upendo, mshikamano, na nia mpya ya kujitoa kwa ajili ya ustawi wa kila mmoja wetu"

 Kwani anasema  kuwa maendeleo ni matokeo ya juhudi za pamoja, maono ya pamoja, na imani kuwa kwa kushikamana, tunaweza kuyafikia

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI