Alexander Pichushkin, muuaji hatari wa Urusi aliyefungwa maisha mwaka 2007 kwa kuua watu 48, amesema yuko tayari kukiri mauaji mengine 11, idara ya mahakama ya Urusi ilisema Jumamosi.
Kwa mujibu wa Reuters Pichushkin, ambaye sasa ana umri wa miaka 50, alilenga mara nyingi watu wasio na makazi, walevi na wazee, karibu na Bitsevsky Park, mahali penye mandhari ya kijani kibichi kusini mwa Moscow.
Mauaji hayo yalifanyika katika kipindi cha kutoka 1992 hadi 2006.
Alipewa jina la utani "muuaji wa chessboard" na vyombo vya habari vya Urusi kwa sababu aliwaambia wapelelezi katika kukiri kwake kwamba alikuwa na mpango wa kuweka sarafu kwenye kila ubao wa kila muathirika wa vitendo vyake.
Pichushkin amekuwa akishikiliwa katika gereza la Polar Owl, katika eneo la Arctic kaskazini mwa Urusi, tangu ahukumiwe.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Telegram siku ya Jumamosi, Idara hiyo ya Urusi ilisema kuwa Pichushkin aliwaambia wapelelezi kuwa yuko tayari kukiri mauaji 11 zaidi ya wanaume na wanawake.
Pichushkin kwa muda mrefu amekuwa akishukiwa kwa mauaji zaidi ya yale ambayo alihukumiwa.
Wakati wa kesi yake alidai kuua watu 63, lakini waendesha mashtaka walimshtaki kwa mauaji 48 na majaribio matatu ya kuua.
0 Comments