Na Shemsa Mussa -Matukio daima - KAGERA.
Kwa mwaka wa fedha 2024-2025 Halmashauri ya Bukoba tumepokea fedha za maendeleo Katika sekta mbali mbali hivyo Hatuna budi kuendelea kumshukuru Mhe Ris wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na Mwandishi wetu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg Jacob Nkwera akiwa ofisini kwake amesema katika upande wa shule za Misingi na awali Halmashauri imepokea fedha za maendeleo Katika shule Nne na Kila shule imepokea Shilingi Million 63 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili pamoja na ujenzi wa Matundu 8 ya vyoo kwa Kila shule,Amezitaja shule zilizopokea fedha hizo katika awamu hiyo ya kwanza kuwa ni kyakailabwa,Buyekera,Kitendaguro ,pamoja na Kahororo zote zikiwa shule za Misingi na awali.
Bw Nkwera amesema katika shule za sekondari Halmashauri imepokea Shilingi Million 100 kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu (two in one) katika shule ya sekondari Kyamigege,pia waliweza kupokea fedha Shilingi Million 584 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya ijuganyondo ,Maabara pamoja na nyumba za walimu na zote zipo katika hatua za ukamilishaji.
Amesema wameweza kupokea fedha kutoka kwa wafadhili (Bark gold) kwa ajili ya ujenzi Mabweni mawili,Madarasa matano pamoja na Matundu nane ya vyoo,pia Halmashauri imepokea fedha Shilingi Million 130 kwa ajili ya ukamilishaji wa bwaro la wanafunzi katika shule ya sekondari kagemu.
" Bado tunamshukuru Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia miradi mingi na yenge thamani nyingi ya fedha miradi ya (Tactic)fedha za miradi hiyo tutakamilisha stend yetu ya Mabasi makubwa ,Barabara zetu Hapa mjini na zimepokelewa fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa stend ya Magari madogo. ,ujenzi wa kingo za Mto yenye urefu wa kilometers 7.3 pamoja na taa za Barabarani zaidi ya taa 413 zitawekwa hapa mjini, amesema Bw Nkwera "
Ameongeza kuwa ipo mikakati ya ujenzi wa soko kubwa kwa ajili ya Wafanyabiashara wadogo wadogo( Machinga ) katika eneo la Machinjioni na amesema wapo katika hatua za mwisho ili ujenzi uanze na lengo ni kuwapatia Machinga wote eneo kwa ajili ya kufanya kazi zao kwa uhakika hasa wale ambao wanafanya kazi hizo katika maeneo ambayo sio lasmi na wale ambao hawana maeneo kabisa.
Aidha Bw Nkwera amesema katika upande wa Afya wameshapokea Shilingi Million 215 kwa ajili kuendeleza ujenzi katika hospital ya manispaa ya Bukoba,kwa jengo la upasuaji,Mama na Mtoto,Mateneti,jengo la kufulia ,Word za Wanawake, wanaume na watoto, jengo la mionzi( X-ray),jengo la upasuaji pamoja na chumba Cha kuhifadhi Maiti ambapo kina uwezo wa kuhifadhia miili 12 kwa wakati mmoja.
"ila pia hata sisi kama watumishi wa Manispaa tumekumbukwa tumepatiwa fedha Shilingi Million 700 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala kama unavyoona jengo letu limechakaa sana na hiyo fedha ni kianzio ila jengo Zima litachukua ghalama ya Shilingi Billion 4 Hadi 4.5 pamoja na thamani zake ndani,na vilevile hapa Manispaa yetu Kuna utoaji wa Mikopo kwa Wanawake,vijana na watu wenye ulemavu awamu ya kwanza imefunguliwa Mwezi Januari na dirisha litafungwa 25 April 2025 kwa ajili ya maandalizi ya awamu ya pili,ameongeza Bw Nkwera"
Pia ametoa Rai kwa wananchi wote kuheshimu na kutunza miradi yote ikiwa lengo la Serikali ni miradi hiyo iweze kutoa huduma na kulahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka,huku akisema licha ya Serikali kujenga miradi ila miradi hiyo ni ya wananchi hivyo ni wajibu wa Kila mwananchi kuwa barozi mzuri katika kutunza miradi hiyo ili iendelee kutoa huduma endelevu kwa Sasa na baadae.
0 Comments