Header Ads Widget

"MIUJIZA" MTOTO WA KWANZA KUZALIWA UINGEREZA KUPITIA KUPANDIKIZWA KWA KIZAZI

 


Mtoto Amy Isabel aliyepigwa picha mara baada ya kuzaliwa

Mtoto wa kike anayechukuliwa kuwa "muujiza" amekuwa wa kwanza nchini Uingereza kuzaliwa na mama kupitia njia ya kupandikizwa kwa kizazi.

Mama wa mtoto huyo, Grace Davidson, 36, alizaliwa bila tumbo la uzazi, na dadake akamsaidia na tumbo lake mnamo mwaka 2023 - katika kile ambacho wakati huo kilikuwa upandikizaji pekee wa uzazi uliofaulu nchini Uingereza.

Miaka miwili baada ya operesheni hiyo ya kwanza kuwahi kufanyika, Grace alijifungua mtoto wake wa kwanza mwezi wa Februari. Yeye na mumewe, Angus, 37, wamempa binti yao jina la dada yake Amy, ambaye alitoa tumbo lake la uzazi.

Kumbeba mtoto Grace - ambaye alikuwa na uzani wa zaidi ya kilo mbili kwa mara ya kwanza ilikuwa jambo la "kipekee" na "kufurahisha", mama Grace alisema.

"Haikuwa rahisi kwetu kwa sababu hatukuwahi kufikiria kwamba hili lingewezekana," anasema.

Grace na Angus, ambao wanaishi kaskazini mwa London lakini wanatoka Scotland, wanatumai kupata mtoto wa pili kwa kutumia tumbo la uzazi lililopandikizwa.

Awali wanandoa hao walitaka kusalia bila kujulikana, lakini kufuatia kuzaliwa salama kwa mtoto Amy sasa wamezungumza na BBC kuhusu "muujiza" huo uliotokea.

Timu ya upasuaji iliiambia BBC kuwa wamefanya upandikizaji wa uzazi mwingine mara tatu kwa kutumia tumbo la uzazi l a waliofariki ambao walikuwa wameridhia tangu kupandikizwa kwa Grace.

Wanalenga kutekeleza jumla ya upandikizaji 15 kama sehemu ya majaribio ya kimatibabu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI