Header Ads Widget

MAZISHI YA PAPA FRANCIS YATAFANYIKA JUMAMOSI HUKU VATICAN IKITOA PICHA ZA JENEZA LAKE LA WAZI

 

Papa Francis, 88, alifariki siku ya Jumatatu baada ya kupatwa na kiharusi na mshtuko wa moyo na atazikwa siku ya Jumamosi kulingana na Vatikan.

Papa alikaa hospitalini kwa wiki tano mapema mwaka huu akiugua nimonia mara mbili. Lakini alirudi Vatikani karibu mwezi mmoja uliopita na alionekana kupata nafuu, akitokea katika Uwanja wa St. Peter's Square Jumapili ya Pasaka.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mwili wake utapelekwa katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro siku ya Jumatano asubuhi, katika msafara utakoongozwa na makadinali, pkuruhusu waumini kutoa heshima zao za mwisho kwa Papa.

Ibada ya mazishi yake itafanyika katika Uwanja wa St. Peter's Square, Jumamosi asubuhi.

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alizozana mara kwa mara na papa kuhusu uhamiaji, alisema yeye na mkewe watasafiri kwa ndege hadi Roma kwa ajili ya ibada hiyo.

Miongoni mwa wakuu wengine wa nchi wanaotarajiwa kuhudhuria ni Javier Milei, rais wa Argentina asilia ya Francis, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, kulingana na chanzo katika ofisi yake.

Kwa nini Wakatoliki wana majeneza yaliowazi

Vatican imetoa picha za jeneza la Papa Francis lililowazi lililovishwa mavazi mekundu kwenye kanisa la Casa Santa Marta, kulikokuwa nyumbani kwake wakati akihudumu kwama papa kwa miaka 12.

Picha hizo pia zinaonyesha Kardinali Kevin Joseph Farrell akibariki mwili wa marehemu Papa wakati wa ibada ya wafu.

Majeneza yaliyowazi ni kawaida katika mazishi ya Katoliki, ambayo kawaida ni sherehe za kiibada - lakini sio hitaji la lazima.

Wanaruhusu wapendwa kuona marehemu kwa mara ya mwisho kabla ya mazishi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI