Header Ads Widget

WABUNGE WA UINGEREZA WANATAKA KUMZUIA TRUMP KUHUTUBIA BUNGENI WAKATI WA ZIARA YAKE

 Rais wa Marekani, Donald Trump akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer katika Ikulu ya White House mwezi Februari.

Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Uingereza, wametoa wito wa kutaka rais wa Marekani, Donald Trump azuiwe kuhutubia bunge atakapozuru Uingereza.

Rais huyo wa Marekani amesema Kasri la Buckingham "linapanga tarehe katika mwezi Septemba" ili yeye aende Uingereza.

Lakini baadhi ya wabunge wameelezea wasiwasi wao kuwa "haitafaa" kwake kuzungumza katika Bunge la Westminster kama watangulizi wake Barack Obama, Ronald Reagan na Bill Clinton walivyofanya.

Iliripotiwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la Times, ujumbe uliotumwa kwa Lord McFall wa Alcluith, spika mkuu, ukisema: "Ikiwa itapendekezwa kwamba aalikwe kuhutubia Mabunge yote mawili, ninatumai wewe na Lindsay mtaeleza kwamba hilo halitofaa kwa sasa kwa sababu ya mtazamo wake kuhusu Uingereza, demokrasia ya bunge, muungano wa Nato na Ukraine."

Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la Uingereza, juhudi za kumzuia Trump kuhutubia wabunge zinaratibiwa na Lord Foulkes, Waziri katika serikali ya zamani ya Sir Tony Blair.

Foulkes amesema: “Wakati serikali inawajibika kuzungumza na serikali za kila aina, bunge halipaswi kumkaribisha kiongozi ambaye anapinga demokrasia na kudharau mahakama na utawala wa sheria."

"Pia anashindwa kulaani uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, ambao pande zote katika bunge la Uingereza zimelaani."

Wakati huo huo, mbunge wa chama cha Labour Kate Osborne anasemekana kumtaka spika wa bunge la Commons, Lindsay Hoyle, kufuata njia ya mtangulizi wake John Bercow kupinga hotuba ya rais huyo.

Baadhi ya marais wa Marekani ambao wameshafanya ziara ya kiserikali na kunywa chai au chakula cha mchana na Ufalme wa Uingereza, ni George W Bush na Obama.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI