Header Ads Widget

MASHAMBULIZI YA ISRAELI KWENYE SHULE YA GAZA YAUA 27 - HAMAS


 

Takriban Wapalestina 27 wameuawa katika shambulizi la angani lililofanywa na Israel katika shule moja kaskazini mwa Gaza iliyokuwa ikitumika kama hifadhi ya familia zilizopoteza makazi, wizara ya afya inayoongozwa na Hamas imesema.

Makumi zaidi walijeruhiwa wakati shule ya Dar al-Arqam katika wilaya ya kaskazini-mashariki ya Tuffah ya Jiji la Gaza iliposhambuliwa, ilinukuu hospitali ya eneo hilo kusema.

Jeshi la Israel limesema liliwashambulia "magaidi mashuhuri waliokuwa katika kituo kikuu cha udhibiti cha Hamas" katika mji huo, bila kutaja shule.

Wizara ya afya hapo awali iliripoti kuuawa kwa watu wengine 97 katika mashambulizi ya Israel katika muda wa saa 24 zilizopita, huku Israel ikisema mashambulizi yake ya ardhini yanapanuka ili kuteka maeneo makubwa ya ardhi ya Palestina.

Msemaji wa wakala wa Ulinzi wa Raia wa Gaza unaoendeshwa na Hamas, Mahmoud Bassal, alisema watoto na wanawake ni miongoni mwa waliofariki kufuatia shambulizi la shule ya Dar al-Arqam.

Pia alisema mwanamke ambaye alikuwa na ujauzito mkubwa wa mapacha alipotea pamoja na mumewe, dadake na watoto wake watatu.

Video kutoka hospitali ya karibu ya al-Ahli ilionyesha watoto wakikimbizwa ndani ya magari na lori wakiwa na majeraha mabaya.

Taarifa kutoka kwa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) ilisema eneo la mji wa Gaza ambalo lilishambuliwa lilitumiwa na wapiganaji wa Hamas kupanga mashambulizi dhidi ya raia na wanajeshi wa Israel.

Imeongeza kuwa hatua nyingi zimechukuliwa kupunguza madhara kwa raia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI