Header Ads Widget

KIRIGINI AMPONGEZA RAIS DKT.MWINYI KUSIMAMIA MISINGI YA UONGOZI WA HAYATI RAIS ABEID AMANI KARUME

 


Na Shomari Binda-Musoma 

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussen Ally Mwinyi amepongezwa kwa kusimamia misingi ya uongozi uliofanywa na Hayati Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume.


Pongezi hizo zimetolewa na kada wa Chama cha Mapinduzi( CCM) na Mjumbe wa zamani wa (NEC) Paul Herman Kirigini.


Akizungumza kwa njia ya simu na Matukio Daima leo aprili 7,2025 katika kumbukizi ya miaka 53 tangu kifo cha Hayati Karume amesema moja ya misingi hiyo ni kuwaletea maendeleo wananchj wa Zanzibar.



Amesema tangu serikali ya awamu ya 8 ya Dkt.Mwinyi iingie madarakani yameshuhudiwa mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwenye visiwa vya Zanzibar.


Kirigini amesema moja ya kumbukumbu ya hutuba za Hayati Shekh Abeid Amani Karume ni vijana kujiandaa kuja kuwaongoza wananchi na kuwaletea maendeleo wananchi jambo linalofanywa vyema na Rais Dkt.Mwinyi.


Amesema ujenzi wa skuli kwaajili ya maendeleo ya elimu zimekuwa zikijengwa na kushuhudiwa ufunguzi wake mara kwa mara.


Kirigini pia amezungumzia miradi mingine mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi ambayo pia imeonekana ikifunguliwa na kuzinduliwa kwenye visiwa vya Zanzibar.


" Tunapomkumbuka leo Mzee wetu Hayati Rais Abeid Amani Karume miaka 53 ya kifo chake tupongeze namna Rais Dkt.Hussen Ally Mwinyi anavyoishi na maono yake.


" Maendeleo kwa wananchi yalikuwa malengo ya Hayati Karume na leo tunashukuru tukiona leo mambo mazuri yanaonekana katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar",amesema.


Aidha Kirigini ametoa wito kwa vijana na wanaopata nafasi ya kuaminiwa kwenye nafasi za uongozi kuzisimamia vyema na kuwaletea wananchi maendeleo.


Leo aprili 7,2025 ni kumbukizi ya kifo cha Sheikh Abeid Amani Karume, aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar na mmoja wa waasisi wa Muungano wa Tanzania.

 Leo tunamkumbuka kama kiongozi aliyeacha alama ya kudumu katika historia ya Zanzibar na Tanzania.


Anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika historia ya Zanzibar hasa baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964, yaliyomng’oa Sultani na kuanzisha serikali madhubiti.


 Miongoni mwa mambo makubwa aliyoyatekeleza ni kushiriki katika kuunda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa Tanzania mwaka huo huo hatua iliyoleta mshikamano wa kitaifa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI