Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania (SACP) William Mkonda akitoa onyo kwa Madereva wasiotaka kufuata sheria za usalama barabarani na kusababisha ajali zinazopelekea vifo na majeruhi kwa Watanzania.
Kamanda Mkonda ameyasema hayo Aprili 04, 2025 alipotembelea Mkoani Kilimanjaro katika maeneo zilipotokea ajali mbili tofauti Ugweno Wilayani Mwanga na Chome Wilayani Same, ajali ambazo zimesababisha vifo vya watu 15 na majeruhi zaidi ya 50 ndani ya wiki moja Machi 30 na April 3, 2025.
0 Comments