Katika mfululizo wa makala zangu juu ya uchambuzi wa majimbo haya matatu, Bukene, Nzega vijijini na Nzega Mjini, nimekuwa nikijitahidi kuwasemea wapiga kura ambao mimi pia ni mmojawapo.
Nia hasa ni kujaribu kufikisha ujumbe wa nini tunatarajia kutoka katika chama chetu cha Mapinduzi (CCM) na hasa kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.
Nimerudia mara kadhaa kusema wananchi wamechoshwa na rushwa, ufisadi, na kuishi na kero lukuki ambazo zinaweza kutatuliwa bila ya kuhangaika sana kama uondoshwaji wake ukisimamiwa ipasavyo.
Shida inayojitokeza hapa ni kwamba kero hizo zote zimekuwa zikichangiwa kwa kiasi kikubwa na watu waliotakiwa kuwa watatuzi wa kero hizo lakini wanashindwa kwa sababu wao wenyewe wamekuwa sehemu ya kero na matatizo hayo.
Sehemu ya kwanza ya makala haya nilieleza nitataja miongoni mwa mambo aliyoyaahidi bwana Hussein Bashe wakati anaomba ubunge mwaka 2015 na mwaka 2020, na katika makala haya nitataja moja tu la Elimu.
Suala la elimu, bwana Hussein Bashe wakati wa kampeni aliahidi kusimamia, kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu mashuleni tangu shule ya msingi hadi kidato cha sita, na akaahidi kuwalipia ada wanafunzi wote watakaofaulu kwenda kidato cha tano na sita ambao watatokana na jimbo la Nzega Mjini.
Tangu 2015 shule nyingi za msingi na sekondari hapa Nzega hazina waalimu wa kutosha na leo ni miaka 10 sasa.
Hapa ndipo linaibuka swali, kwamba hivi huyu bwana Hussein Bashe alijua alichokiahidi lakini bila mbinu ya kufikia mafanikio hayo au aliahidi anachokijua kuwa haiwezekani ili kuwalaghai wananchi wampigie kura tu?
Unaahidi vipi kumsomesha mwanafunzi wa "kidato cha tano na sita" ilihali unajua shule hazina walimu wa kutosha? Mwanafunzi atafaulu vipi bila waalimu?
Cha kushangaza na kusikitisha hata wadau wa elimu, bwana Hussein Bashe nao amekuwa akiwazuia kupitia mkurugezi.
Kwa mfano, ndugu Peter Mashili aliombwa na waalimu msaada wa compyuter na mashine za photo copy ili punguza gharama kwa wanafuzi wanaochagishwa pesa na walimu kwa ajili ya copy na limu, Mashili aliguswa sana na changamoto hiyo na akaahidi kuleta compyuter na photo copy mashine shule zote za Halmashauri ya mji wa Nzega.
Lakini Mbunge Hussein Bashe akamtumia Mkurugezi kuzuia msaada huo, shule zimekosa compyuter na photo copy kwa sababu tu Hussein Bashe anayejisifia kuinua elimu na kusomesha wanafunzi lakini anazuia.
Katika mazingira hayo, huyu ni mbunge anayejitambua na kutambua shida za wananchi?
Ni kweli kwamba maendeleo si lazima kwa jamii zote, na wala si jamii zote zinakubaliana kuhusu maana ya dhana hiyo ya maendeleo.
Zipo jamii ambazo zina mtazamo tofauti kabisa na jamii nyingine, na wala haziwezi kumaliza tofauti hizo baina yake kama ilivyo kati ya sisi Nzega na Kahama, sisi Nzega na Igunga.
Lakini kuna mambo machache ambayo tunaweza kukubaliana nayo kwamba haya ni ishara za maendeleo kwa kila mwanajamii; moja kati ya hayo ni elimu inayomfanya kila mtu aishi kikamilifu, na wala si kama zuzu; pili, ni furaha, tatu, ni utangamao na nne ni matarajio ya mambo mema zaidi katika mstakabali wa jamii husika nk.
Sisi Nzega tunalazimishwa kuwa na maisha duni na ya hovyo hovyo na huyu bwana Hussein Bashe, kwa sababu kiongozi anayezuia maendeleo ya jamii huyo siyo kiongozi wa watu bali ni kiongozi wa kikundi cha wajasiriamali wanaojinufaisha wao binafsi, Hussein Bashe ni kati ya viongozi wa hovyo ambao hawafai kuaminiwa na jamii yoyote inayotaka kuendelea kutoka katika maisha duni na umasikini.
Haiwezekani huyu bwana Hussein Bashe, tangu 2010 kila mgogoro uwe ndani ya chama anatajwa yeye kuhusika na mgogoro huo.
Mfano uchaguzi wa mwenyekiti wa CCM Wilaya wa Mama Igoko na Mzee Shija, uchaguzi wa mwenyekiti wa Kanuda na Mwinyimvua, uchaguzi wa mwenyekiti wa Halmashauri awamu zote, uchaguzi wa madiwani na ubunge mlalamikiwa mkuu ni yeye.
Alilalamikiwa kukwamisha hata kununuliwa kwa mitambo ya kuchonga visima na mabarabara wakati wa ubunge wa Dk. Hamis Kigwangalla, matokeo yake fedha ikaishia mifukoni mwa wachache.
Nachotaka kusema hapa ni kwamba wananchi waelewe mtu huyu hana nia njema na maendeleo ya Nzega, wala hajaja hapa kwa ajili ya kuongoza wananchi bali aliletwa na akina Lowassa kwa minajiri yao binafsi ya kifisadi.
Hussein Bashe ni mbabaishaji hafai katika uongozi wa jamii kwa sababu ni mtu wa propaganda na anaifanya kwa kiwango cha hali ya juu na kwa ufundi, ameweza kuwaaminisha watu wengi hasa wasiojitambua kwa kuwaaminisha mambo ya uongo.
Watu hawa wameshaaminishwa kuwa yeye ndiye kila kitu katika maisha yao na amewafanya wayachukulie maisha yao ya hovyo na ya taabu kuwa ndiyo bora.
Wanasiasa aina ya Hussein Bashe ndiyo wamesababisha wananchi wengi kutoiamini CCM kutokana na mfumo wao wa hovyo waliousimika ndani ya chama.
Sina uhakika hawa watu wanaozungumzia mfumo wanamaanisha nini hasa isipokuwa ninachojua na ninachosikia mara kwa mara ni kwamba Chama chetu Cha Mapinduzi (CCM), kina mfumo kiliowekwa ndani ya chama chenyewe na ndani ya Serikali ambao ndiyo kikwazo cha mabadiliko au mageuzi ya kweli katika taifa letu.
Muda wote kabla ya kampeni, wakati wa kampeni na hata baada ya kampeni kumekuwepo na tuhuma dhidi ya CCM kuwa imeweka mfumo ambao unakumbatia maovu, rushwa na ufisadi kiasi kwamba suala la mabadiliko au mageuzi ya kweli ya kuwaondoa wananchi katika dimbwi la umasikini ni kiini macho tu na kamwe hilo haliwezekani.
Wanasiasa aina ya Hussein Bashe ndiyo wamesababisha Chama chetu Cha Mapinduzi kichukiwe na wananchi, na sasa viongozi wetu wa juu wanapata taabu kuhangaika na wanasiasa wa upinzani badala ya kuhangaika na dumuzi ndani ya CCM.
Wananchi wanaona bora matumaini yao wayaelekeze upande wa pili ambako wanaona angalau wajifariji na kuweka matumaini ya mabadiliko.
Ni bora viongozi wa chama chetu waelewe hili kabla hawajaharibikiwa, wasihangaike na vyana vya upinzani, vyama hivi vinaonewa bura kwani wachawi wa matatizo ya wananchi wamo ndani ya CCM.
Na bila shaka wala tashwishwi yoyote ni hawa akina Hussein Bashe, genge ambalo wamelirithi kutoka kwa Lowassa na Lostam ndiyo limepoka madaraka ya chama chetu.
Kwiyeya Singu. 0784977072
0 Comments