Header Ads Widget

HATIMAYE PAPA FRANCIS AZIKWA MAZIKO YA SIRI NJE YA VATICAN

 

Mwili wa Francis umezikwa katika kanisa la Santa Maria Maggiore huko Roma.

Katika taarifa, Vatican imesema jeneza la Papa Francis limezikwa katika Basilika la Santa Maria Maggiore katikati ya Roma.

Anakuwa Papa wa kwanza tangu Leo XIII, aliyefariki mwaka 1903, kuzikwa nje ya Vatican.

"Papa ni wa kwanza katika zaidi ya karne moja kuzikwa nje ya Vatican, na mazishi yake yalikuwa ya faragha, yakiwaruhusu wale walio karibu naye kutoa heshima zao," taarifa hiyo imeongeza.

Kila mara Francis aliporudi Roma baada ya safari ya nje ya nchi, alitembelea Santa Maria Maggiore.

Ni chaguo linalofaa embalo Francis alikuwa amejitolea sana kwa Bikira Maria, na Santa Maria Maggiore lilikuwa kanisa la kwanza kuwekwa wakfu kwa ajili yake lilipojengwa katika karne ya 4.

Kabla ya maziko ya siri, Zaidi ya watu 400,000 walikusanyika kuhudhuria ibada ya mazisi yaka ndani ya uwanja na maeneo yanayozunguka Kanisa hilo.

Aliyeongoza ibada ya mazishi alikuwa Dekano wa Chuo cha Makadinali, Kardinali Giovanni Battista Re, Muitalia mwenye umri wa miaka 91 ambaye alipata upadrisho katika Jimbo la Brescia mwaka 1957 na Mwaka 2001, Papa John Paul II alimteua kuwa kardinali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI