Header Ads Widget

DC CHIKOKA AMUWAKILISHA DKT.SAMIA KUSHEREHEKEA EID EL FITR NA WATOTO WENYE UHITAJI

 

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amemuwakilisha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitr na watoto wenye uhitaji.

Chikoko ameshiriki na watoto wanaolelewa na kutunzwa kwenye kituo cha ST.Justine kilichopo Kata ya Makoko mjini hapa.

Licha ya mkuu huyo wa Wilaya sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma mjini Benedict Magiri, Meya Patrick Gumbo,Katibu wa UWT Wilaya ya Musoma mjini Teddy na walezi wa kituo hicho.


Akizungumza na watoto hao baada ya kukabidhi zawadi zilizotolewa na Rais Dkt.Ssmia na kula nao chakula Dc Chikoka amesema Rais anawapenda na anawatakia sikukuu njema.



Amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anao upendo mkubwa na ndio sababu amewafikia na kuwapa zawadi mbalimbali za Eid El Fitr.


" Mama yetu Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan anawapenda sana na ameniagiza nije kuwaletea zawadi za sikukuu.


" Tuendelee kumuombea Rais wetu awe na afya njema na aendelee kuwahudumia wananchi na watoto wetu hawa",amesema.


Viongozi walioambarana na mkuu huyo wa Wilaya kwenye kituo hicho wamemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa upendo aliowaonyesha watoto hao wakiwemo yatima na wenye ulemavu mbalimbali.


Kwa upande wao walezi wa kituo hicho pia wamemshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwafikia kupitia mkuu wa Wilaya na kuwapa zawadi mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI