
Algeria imewataka wafanyakazi 12 wa ubalozi wa Ufaransa kuondoka nchini humo ndani ya saa 48, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amesema.
Jean-Noel Barrot aliongeza kuwa hatua hiyo inahusishwa na kufunguliwa mashitaka dhidi ya Waalgeria watatu nchini Ufaransa siku ya Ijumaa, mmoja wao akiwa afisa wa ubalozi.
Wanatuhumiwa kuhusika katika tukio la mwaka jana la utekaji nyara wa Amir Boukhors, 41, mkosoaji wa serikali ya Algeria, ambaye inasemekana alipewa hifadhi nchini Ufaransa mwaka 2023.
Barrot aliitaka Algeria "kuachana" na kufukuzwa na akasema Ufaransa iko tayari "kujibu mara moja" ikiwa wataendelea.
Boukhors, anayejulikana pia kama Amir DZ, ameishi Ufaransa tangu 2016 na aliripotiwa kupata hifadhi ya kisiasa mnamo 2023.
Alitekwa nyara mnamo Aprili 2024 katika vitongoji vya kusini mwa Paris na kuachiliwa siku iliyofuata, kulingana na wakili wake Eric Plouvier.
Plouvier aliiambia shirika la habari la AFP kwamba Boukhors "amekabiliwa na mashambulizi mawili makubwa, moja mnamo 2022 na lingine jioni ya Aprili 29 2024".
Vyombo vya habari vya Ufaransa viliripoti kuwa alilazimishwa kuingia kwenye gari lililokuwa na watu waliodaiwa kuwa "maafisa bandia wa polisi", kisha akaachiliwa siku iliyofuata bila maelezo.
0 Comments