Header Ads Widget

AJALI YA BASI MUSOMA ,ABIRIA WANUSURIKA KIFO

 

Na Shomari Binda-Musoma 

ABILIA waliokuwa wakisafiri na basi la Spider aina ya Tata lenye namba za usajili T 703 DDS kutoka Musoma mjini kuelekea Musoma Vijijini wamenusulika kifo baada ya basi hilo kupinduka jana jioni.


Basi  hilo liliacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Murunyigo Kata ya Ifulifu ambapo mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo wamedai dereva wa gari hilo alikuwa mwendo kasi.


Wakizungumza na Matukio Daima eneo la ajali hiyo mashuhuda hao wamesema mwendo  ulikuwa  si wa kistarabu ndio uliopelekea gari hilo kupinduka.

Juma Katundu mmoja wa walioshuhudia ajali hiyo amesema madereva wa njia hiyo wamekuwa wakiendesha mwendo kasi na kuomba jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani kuongeza nguvu kw3nye njia hiyo.

" Madereva njia hii ya Majita wanaendesha kwa kasi sana huku wakiwa wanafukuzana kuwahi abilia hii ni hatari sana.

" Hili ni bus la pili kwa siku za hivi karibuni kupinduka lakini tunaehukuru Mungu hakuna vifo vilivyotokea eneo la ajali hatujui wakati wakipewa huduma",amesema.

Akizungumza kwa njia ya simu kuhusiana na ajali hiyo,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Mara Mrakibu wa Polisi Adribert Ntilicha amesema hakuna kifo kilichotokea kwenye ajali hiyo na majeruhi wanne wanapatiwa huduma hospitalini.

Amesema.jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa kilichopelekea kutokea kwa ajali hiyo huku akitoa wito kwa madereva kuwa makini wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.

Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo ametoa pole kwa wanusulika wa ajali hiyo na kuwaombea Mungu wapone na kurejea kwenye majukumu yao.



TAZAMA FULL VIDEO MEDALA HIGH SCHOOL

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI