Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati Jeshi la polisi mkoa wa Njombe likiwakamata watu 25 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ya uhalifu katika kipindi cha mwezi machi matukio ya wizi kwa kutumia usafiri wa pikipiki yameendelea kuripotiwa na kuchafua taswira ya bodaboda na kurudisha nyuma jitihada za wananchi kujiingizia kipato.
Hivi karibuni Jeshi la Polisi liliripoti kuwakamata baadhi ya vijana huko Nundu wakituhumiwa kutumia pikipiki kukwapua simu za wananchi,Matukio yanayoendelea kutokea ndani ya mkoa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga anasema safari hii Jeshi hilo limewakamata watu wengine wawili Ally Mtate na Dickson Mgaya Fundi simu wakitumia pikipiki kupora simu huku likitoa onyo kali kwa wahalifu.
Ben Kapole,Longnus Hongoli na Devis Mwenda ni baadhi ya madereva bodaboda mjini Njombe ambao wanalaani vikali vitendo vya wizi wa kutumia pikipiki vinavyofanywa na watu ambao wakati mwingine sio maofisa usafirishaji kwani vinawachafua na kuwarudisha nyuma kiuchumi.
Ili kujua mikakati na udhibiti wa matukio hayo Kwa njia ya simu kituo hiki kimezungumza na Mwenyekiti wa Bodaboda wilaya ya Njombe Bwana Veremund Msigwa ambaye amesema wamekuwa wakishirikiana na jeshi la Polisi kupambana na wahalifu hao huku akisema wameanza zoezi la ugawaji wa namba za bodaboda kwenye vituo ambao ni wanachama wao kwa lengo la kurahisisha wateja wanapokodi pikipiki.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo mkoa wa Njombe una zaidi ya pikipiki 6000 zilizosajiliwa na kufanyakazi ya bodaboda huku katika mji wa Njombe kukiwa na Pikipiki 1483.
0 Comments